settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu kuwa mama Kristo?

Jibu


Kuwa mama jukumu la muimu sana ambalo Mungu alilichagua kulipa wamama wengi. Mama Mkristo ameambiwa kuwa awapende watoto wake (Tito 2: 4-5), katika sehemu ili asilete shutuma kwa Mungu na Mwokozi ambaye kwa jina lake abeba jukumu.

Watoto ni tuzo kutoka kwa Bwana (Zaburi 127:3-5). Katika Tito 2:4, neno la Kiyunani philoteknos laonekana kuwaambia wamama wawapenda wana wao. Hili neno linadhihirisha “upendo wa mama” maalumu. Dhana ambayo yotoka katika maneno haya ni ile ya ulezi wa watoto wetu, kwa upendo kuwakumbatia, kutimiza mahitaji yao, kwa ukarimu kufanya urafiki na kila mmoja kama tuzo la ajabu kutoka kwa Mungu.

Mambo mengi yameamuriwa kwa wamama Wakristo katika neno la Mungu:

Kuwa karibu- Asubuhi, mchana na hata usiku (Kumbukumbu La Torari 6:6-7)

Husisha- kutangamana nao, kujadiliana nao, kuwaza nao na kusukuma maisha pamoja (Waefeso 6:4).

Kuwafunza- maandiko na mitazamo ya Kibibilia (Zaburi 78:5-6; Kumbukumbu La Torati 4:10; Waefeso 6:4)

Kuwaelekeza- mzaidie mtoto kukuza ujuzi na kugundua uwezo wake (Methali 22:6) na karama za roho (Warumi 12:3-8 na 1 Wakorintho 12).

Kurudi- kuwafunza kumcha Mungu, kuwa na msimamo kila wakati, kuwa wa upendo na wenye msimamo imara (Waefeso 6:4; Waebrania 12:5-11; Methali 13:24; 19:18; 22:15; 23:13-14; 29:15-17)

Kutunza- kuwapa masingara ya usemi wa kila wakati, uhuru wa kuanguka wanachokifanya, kuwakubali, upendo usio wa masharti (Tito 2:4; 2 Timotheo 1:7; Waefeso 4:29-32; 5:1-2; Wagalatia 5:22; 1 Petero 3:8-9).

Kuwa mfano mwema kwa maadili- kuishi chenye unasema, kuwa kielelezo kutoka kwacho mtoto ataweza kujifunza kwa “kushika” hizi tabia za kuishi maisha ya uungu (Kumbukumbu La Torati 4:9, 15, 23; Methali 10:9; 11:3; Zaburi 37:18, 37).

Bibilia kamwe haitaji kuwa kila mwanamke lazima awe mama. Ingawa, huwa yasema kwamba wale ambao Mungu amewabariki kuwa wamama lazima wajukue majukumu yao bila mchezo. Wamama wako jukumu la ajabu na la muimu katika maisha ya watoto wao. Uzazi wa mama sio wa kuchosha au kazi isiyofurahisha. Vile mama anavyomzaa mtoto wakati wa uja uzito, na kama vile mama anavyomnyonyesha na kumlea mtoto akiwa mchanga, kwa hivyo wamama wanatekeleza jukumu linaloendelea katika maisha ya watoto wao, hata kama wamefika umri wa kubalehe, ujana, na utu uzima au utu uzima wakiwa na watoto wao. Huku ikiwa ni jukumu la mama lazima libadilishwe na liansishe, upendo, ulezi, utunzi, na utiaji moyo mama anaowapa watoto kamwe usikome.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu kuwa mama Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries