Swali
Je! Wasamaria walikuwa nani?
Jibu
Wasamaria walimiliki nchi zamani ilikuwa ya kabila la Efraimu na nusu ya kabila la Manase. Mji mkuu wa nchi ulikuwa Samaria, zamani mji mkuu na bora. Wakati makabila kumi yalipelekwa mateka huko Ashuru, mfalme wa Ashuru alituma watu kutoka Kutha, Ava, Hamathi, na Sefarvaimu kukaa Samaria (2 Wafalme 17:24; Ezra 4:2-11). Wageni hawa walioaana na watu wa Israeli ambao bado walikuwa ndani na karibu na Samaria. Hawa "Wasamaria" mara ya kwanza waliabudu sanamu za mataifa yao wenyewe, lakini wakiwa wanasumbuliwa na simba, walidhani ni kwa sababu hawakuheshimu Mungu wa eneo hilo. Basi, kuhani wa Kiyahudi alitumwa kwao kutoka Ashuru kuwafundisha katika dini ya Kiyahudi. Walifundishwa kutoka kwa vitabu vya Musa, lakini bado walishikilia mila zao nyingi za ibada za sanamu. Wasamaria walikubali dini ambayo ilikuwa mchanganyiko wa Uyahudi na ibada ya sanamu (2 Wafalme 17:26-28). Kwa sababu Waaisraeli wenyeji wa Samaria walikuwa wameoana na wageni na waliasili dini yao ya ibada ya sanamu, Wasamaria walikuwa kwa ujumla wanazingatiwa kuwa "chotara" na walikuwa wakidharauliwa na Wayahudi kilimwengu.
Sababu zingine za uadui kati ya Waisraeli na Wasamaria zilikuwa zifuatazo:
1. Wayahudi, baada ya kurudi kwao kutoka Babeli, wakaanza kujenga upya hekalu yao. Wakati Nehemia akijishughulisha na kujenga kuta za Yerusalemu, Wasamaria walijitahidi kusimamisha kazi (Nehemia 6:1-14).
2. Wasamaria walijijengea hekalu yao wenyewe juu ya "Mlimani Gerizimu," ambayo Waasamaria walisisitiza kuwa ilichaguliwa na Musa kama mahali ambapo taifa linapaswa kuabudu. Sanballat, kiongozi wa Wasamaria, aliweka mkwe wake, Manasse, kama kuhani mkuu. Hivyo dini ya ibada ya sanamu ya Wasamaria iliendelea.
3. Samaria ikawa mahali pa kukimbilia kwa maharamia wote wa Yuda (Yoshua 20:7; 21:21). Waasamaria walipokea kwa hiari wahalifu wa Kiyahudi na wakimbizi kutoka kwa haki. Wavunja sheria za Kiyahudi na wale waliokuwa wametengwa walipata usalama kwa wao wenyewe huko Samaria, na kuongezeka sana chuki iliyopo kati ya mataifa haya mawili.
4. Wasamaria walipokea vitabu vitano tu vya Musa na kukataa maandishi ya manabii na desturi zote za Kiyahudi.
Kutoka kwa sababu hizi kulitokea tofauti zisioweza kupatanishwa kati yao, hivyo kwamba Wayahudi waliona Waasamaria kuwa watu wabaya Zaidi ya jamii ya binadamu (Yohana 8:48) na hawakuwa na uhusiano nao (Yohana 4:9). Licha ya chuki kati ya Wayahudi na Wasamaria, Yesu alivunja vikwazo kati yao, akihubiri injili ya amani kwa Wasamaria (Yohana 4:6-26), na baadaye mitume walifuata mfano Wake (Matendo 8:25).
English
Je! Wasamaria walikuwa nani?