settings icon
share icon
Swali

Je, Kwa nini Mungu anaruhusu wasio na hatia kuteseka?

Jibu


Kuna mateso mengi ulimwenguni, na kila mtu huyapitia kwa viwango tofauti. Wakati mwingine, watu huteseka kwa sababu ya uchaguzi wao mbaya, matendo ya dhambi, au kutowajibika kimakusudi; katika visa hivi tunaona ukweli wa Mithali 13:15, "Njia ya waovu ni ya taabu." Lakini vipi kuhusu waathiriwa wa hila? Vipi kuhusu wasio na hatia ambao huteseka? Mungu angewezaje kuyaruhusu haya?

Ni asili ya binadamu kujaribu kupata uhusiano kati ya tabia mbaya na hali mbaya, na kinyume chake, kati ya tabia nzuri na baraka. Ile hali ya kutaka kuhusisha dhambi na mateso ni ya msukumo sana hivi kwamba Yesu aliishughulikia mara mbili. "Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.

Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake" (Yohana 9:1-3). Wanafunzi walikosea kudhani kwamba watu wasio na hatia hawawezi kuteseka na walilaumu kipofu huyo (au wazazi wake). Yesu alikosoa fikra zao huku akisema, "haya yalitendeka ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake" (mstari wa 3). Hali ya upofu wa mtu huyo haukusababishwa na dhambi ya kibinafsi; badala yake, Mungu alikuwa na kusudi kuu ya mateso hayo.

Wakati mwingine, Yesu aliongea kuhusu vifo vya watu walioaga katika ajali: "Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo" ( Luka 13:4-5). Katika kisa hiki, Yesu kwa mara nyingine alipuuza wazo kwamba janga na mateso husababishwa na dhambi za kibinafsi. Wakati huo huo, Yesu alisisitiza ukweli kwamba tunaishi katika ulimwengu uliojawa na dhambi na athari zake; kwa hivyo kila mtu anapaswa kutubu.

Hii inafanya tuzingatie ikiwa "wasio na hatia" halisi wapo. Kulingana na Biblia, "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Kwa hivyo, hakuna 'asiye na hatia" kwa maana ya kutokuwa na dhambi. Sisi sote tulizaliwa na asili ya dhambi, tuliyorithi kutoka kwa Adamu. Na kama tulivyoona tayari, kila mtu hupitia mateso, haijalishi kwamba mateso hayo yanaweza kuhusishwa na dhambi fulani ya kibinafsi au la. Madhara ya dhambi huathiri kila kitu; ulimwengu ulianguka, na kwa sababu hiyo viumbe vyote huteseka (Warumi 8:22).

Cha kuvunja moyo zaidi ni kuteseka kwa watoto. Watoto kidogo wanakaribia kutokuwa na hatia kama vile tumewahi kuona ulimwenguni na ni vibaya sana kuona wakiteseka. Wakati mwingine, watoto wasio na hatia huteseka kwa sababu ya dhambi za watu wengine: kutotunzwa, kunyanyaswa, uendeshaji wa gari ukiwa umelewa na kadhalika. Katika visa hivi, tunaweza kusema kwamba mateso husababishwa na dhambi za kibnafsi (sio za watoto hao), na tunajifunza somo kwamba dhambi zetu huwaathiri wengine walio karibu nasi. Wakati mwingine, watoto wasio na hatia huteseka kwa sababu ya kile wengine huita "matendo ya mungu": majanga ya asili, ajali, saratani ya watoto, na kadhalika. Hata katika visa hivi, tunaweza kusema kwamba kwa ujumla, mateso ni matokeo ya dhambi, kwa sababu tunaishi katika ulimwengu wemye dhambi.

Habari njema ni kwamba Mungu hakutuacha hapa kuteseka bila sababu. Ndio, wasio na hatia huteseka (ona Ayubu1-2), lakini Mungu anaweza kukomboa mateso hayo. Mungu wetu mwenye upendo ana mpango mzuri wa kutumia mateso hayo kutimiza makusudi yake tatu. Kwanza, anatumia uchungu na mateso ili kutuvuta kwake ili tushikamane naye. Yesu alisema, "ulimwenguni mnayo dhiki" (Yohana 16:33). Majaribu na dhiki sio mambo yasiyo ya kawaida maishani, ni sehemu ya kuwa mwanadamu katika ulimwengu ulioanguka. Katika Kristo tunayo nanga ambayo inatushikilia sana katika dhoruba zote za maisha, lakini kama hatungepitia katika dhoruba hizo tungejuaje hivyo? Ni katika wakati wa kukata tamaa na wakati wa huzuni tunamtafuta, na ikiwa sisi ni watoto wake, tunampata akitungoja, kutufariji na kutusaidia kwa yote hayo. Kwa njia hii, Mungu anadhibitisha uaminifu wake kwetu na kuhakikisha kwamba tunakaa karibu naye. Manufaa zaidi ni kwamba tunapoona faraja ya Mungu katika majaribu, basi tunaweza kufariji wengine kwa njia ile ile (2 Wakorinth 1:4).

Pili, Yeye anadhibitisha kwamba imani yetu ni halisi katika mateso na uchungu ambayo hayawezi kuepukika maishani. Jinsi tunavyoitikia mateso, haswa wakati hatuna hatia,hudhihirisha ukweli wa imani yetu. Walio na imani katika Yesu, "mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu" (Waebrania 12:2), hawataangamizwa na mateso lakini wataibuka kutoka majaribu hayo, na imani imara, wakiwa "wamejaribiwa kwa moto" ili "kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo" (1 Petro 1:7). Waumini hawamtingizii Kristo ngumi zao au kuhoji Mungu, badala yake "wanahesabu ya kuwa ni furaha tupu" (Yakobo 1:2), huku wakijua kwamba majaribu hudhibitisha kuwa wao kweli ni wana wa Mungu. "Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao" (Yakobo 1:12).

La mwisho, Mungu hutumia mateso kuondoa macho yetu kutoka kwa dunia hii na kuyaelekeza kwa ingine. Biblia inatuhimiza kila wakati tusizame katika mambo ya ulimwengu huu bali tutazamie ulimwengu ujao. Wasio na hatia huteseka katika ulimwengu huu, lakini ulimwengu huu na vitu vyote vilivyomo vitapita; ufalme wa Mungu ni wa milele. Yesu alisema, "Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu" (Yohana 18:36), na wanaomfuata hawaoni vitu vya maisha haya, nzuri au mbaya, kama mwisho wa hadithi. Hata mateso ya uchungu tunayovumilia, "si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu" (Warumi 8:28).

Je,Mungu angeweza kuzuia mateso yote? Kwa kweli angeweza. Lakini anatuhakikkishia kwamba "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani, wale aliowaita kadiri ya kusudi lake" (Warumi 8:28).

Mateso-hata kuteseka kwa wasio na hatia- ni sehemu ya "mambo yote" ambayo Mungu hutumia kutimiza makusudi yake mema mwishowe. Mpango wake ni kamilifu, tabia yake ni haina makosa, na wale wanaomwamini hawatasikitishwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Kwa nini Mungu anaruhusu wasio na hatia kuteseka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries