settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Wamormoni wanajiita wenyewe kama Watakatifu wa Siku za Mwisho?

Jibu


Wakati njaa ya uzoefu wa kidini ilifikia kilele miaka ya 1800, ukosefu wa umoja kati ya matawi mbalimbali ya imani ya Kikristo ikawa kizuizi. Mwanamume mmoja aitwaye Joseph Smith alijitokeza kupendekeza uzoefu wake wa dini kama suluhisho. Alijitangaza mwenyewe kuwa ni nabii wa Mungu. Wafuasi walidai kwamba Mungu alirudisha "ukuhani mtakatifu [wa] mitume na wanafunzi wa kale" kwa Joseph Smith. Smith pia alitangaza kuwa katika "siku hizi za mwisho" za ulimwengu, makanisa mengine yote yalikuwa yanashiriki katika uasi na ufunuo wake binafsi (au kwamba wale waliohusika naye) wanaweza kuaminiwa kwa wokovu na maelezo.

Kimsingi kwa jitihada za Joseph Smith na Oliver Cowdery, shirika lililoundwa na kuitwa Kanisa la Yesu Kristo la watakatifu wa siku za mwisho. Jina hilo liliripotiwa kuja kutoka kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Lilikuwa lionyeshe mambo matatu maalum: 1. Yesu Kristo aliiweka kanisa; 2. huduma ya kanisa ilikuwa maalum kwa siku za mwisho za dunia, na 3. kanisa lingekuwa na watakatifu tu wa kweli waliokubaliwa na Yesu Kristo. Jina kama hilo lilionekana la kuvutia sana wakati wa kubadilikabalika kwa mafundisho makubwa. Kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho linasema kwamba kazi yao ni kuanzisha ufalme wa Mungu na kuanzisha mazoea ya dini ya Kikristo kama Mungu alivyotaka. Mambo haya kwa pamoja kawaida yaliitwa "kurejeshwa kwa injili" na yalikuwa sehemu ya harakati ya kurejesha mapema ya karne ya 19.

Kwa mujibu wa Biblia, ni Mungu atakayeanzisha ufalme Wake (Isaya 9: 7). Watakatifu hawajaitwa kufanya hivyo kwa ajili yake. Pia, ikiwa mtu anatazama siku za mwisho kama mwisho wa umri wa dunia, au kama kujumuhisha siku zote zinazofuata huduma iliyokamilika ya Yesu Kristo, hakuna msaada wa kibiblia kwa injili iliyovunjika inahitaji urejesho. Yesu alitangaza kukubaliwa kwa Simoni Petro kuwa Yeye ni kama "Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" kuwa jiwe ambalo Kanisa Lake litajengwa, ambalo "milango ya Kuzimu haitashinda ..." (Mathayo 16:16, 18). Mungu pia anasema kuwa, ingawa wengine wamepotea kutoka kwa ukweli, "msingi imara wa Mungu umesimama" (2 Timotheo 2: 18-19). Aya hizi zinaonyesha hali asili ya kudumu ya kanisa ndani ya mazingira ya Injili. Hakika, katika nyakati za mwisho, uasi utaongezeka (Mathayo 24:11), lakini injili itabaki imara na wale wanaovumilia (Mathayo 24: 13-14).

Kazi ya kweli ya watakatifu wa leo ni kuendelea kutangaza ukweli wa injili ya milele (Yohana 3:16, Marko 16:15) na "shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia ... katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu "(2 Timotheo 1:13).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Wamormoni wanajiita wenyewe kama Watakatifu wa Siku za Mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries