Swali
Je! Ikiwa Mungu anachukia dhabihu itimao watu, ni jinsi gani dhabihu ya Yesu inaweza kuwa fidia ya dhambi zetu?
Jibu
Biblia inaiweka wazi kuwa Mungu anachukia dhabihu inayotumia wanadamu. Mataifa ya kipagani ambayo yaliizunguka Israeli walikuwa na utamaduni wa kuwatoa watu kama dhabihu kama sehemu ya ibada ya miungu ya uwongo. Mungu alitangaza kuwa "ibada" kama hiyo ilikuwa chukizo Kwake na anazichukia (Kumbukumbu 12:31; 18:10). Zaidi yake, dhabihu za kutumia wanadamu inaunganishwa na Agano la Kale ambapo kulikuwa na tamaduni ya kishetani kama vile uchawi na ubashiri, ambazo pia ni chukizo kwa Mungu (2 Wafalme 21:6). Kwa hivyo, ikiwa Mungu anachukia dhabihu itumia wanadamu, ni kwa nini alimtoa Kristo kama dhabihu msalabani na ni jinsi gani dhabihu hiyo itakuwa fidia ya dhambi zetu?
Hamna shaka kwamba dhabihu kwa ajili ya dhambi ilikuwa ya lazima ikiwa watu wangekuwa na tuamine la uzima wa milele. Mungu alianzisha umuhimu wa kumwaga damu ili kufunika dhambi (Waebrania 9:22). Kwa kweli, Mungu mwenyewe alifanya dhabihu ya kwanza kabisa ya mnyama ili kufunika kwa muda dhambi ya Adamu na Hawa. Baada ya kutamka laana juu ya wenzi hawa wa kwanza, Aliua mnyama, akamwaga damu yake na kutoka kwa ngozi yake akawatengezea nguo Adamu na Hawa (Mwanzo 3:21), na hapo kuanzisha kanuni ya dhibihu ya wanyama kwa ajili ya dhambi. Wkati Mungu alimpatia Musa Sheria, kulikuwa na maelezo pana ya jinsi, lini, na ni chini ya hali gani dhabihu ya wanyama ingefanywa Kwake. Hii ilikuwa iendelee hadi Kristo aje kutoa dhabihu kamilifu na ya mwisho ambayo ilifanya dhabihu ya wanyama isihitajike tena. "Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi" (Waebrania 10:3-4).
Kunazo sababu nyingi za ni kwa nini dhabihu ya Kristo msalabani haikiuki katalio dhidi ya dhabihu ya binadamu. Kwanza, Yesu hakuwa mwanadamu wa kawaida. Ikiwa alikuwa, basi dhabihu Yake ingekuwa ile ya muda kwa sababu uhai wa mtu mmoja haungetosha kufunika dhambi za wengi walioishi. Wala hakuna vile mwanadamu wa maisha yaliyo na mwisho anaweza fidia dhambi dhidi ya Mungu asiye na mwisho. Dhabihu pekee inayotosha lazima iwe isiyo na mwisho, kumaanisha kwamba ni Mungu mwenyewe pekee anaweza fidia dhambi za mwanadamu. Ni Mungu mwenyewe pekee Yeye asiye na mwisho, angeweza kulipia deni Yake tuliyokuwa nayo. Hii ndiyo sababu ni kwa nini Mungu alilazimika kuwa mwanadamu na kuishi miongoni mwa wanadamu (Yohana 1:14). Hakuna dhabihu nyingine ingetosha
Pili, Mungu hakumtoa Yesu dhabihu. Badala yake, Yesu, kama Mungu mwanadamu, alijitoa dhabihu. Hakuna yeyote aliyemlazimisha. Aliyatoa maisha Yake kwa hiari, jinsi alivyoiweka wazi kwa kunena: "Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu" (Yohana 10:18). Mungu Mwana alijitoa dhabihu mwenyewe kwa Mungu Baba na hapo akatimiza masharti yote ya Sheria. Kuliko dhabihu za muda, Yesu alijitoa dhabihu mara moja kwa wote ilifuatwa na ufufuo wake. Aliyatoa maisha Yake na kuyapata tena, na hapo akapeana uzima wa milele kwa wale wote watamwamini Yeye ana kukubali dhabihu yake kwa dhambi zao. Aliyafanya haya kwa upendo wake kwa Baba na kwa wale wote Baba amempa (Yohana 6:37-40).
English
Je! Ikiwa Mungu anachukia dhabihu itimao watu, ni jinsi gani dhabihu ya Yesu inaweza kuwa fidia ya dhambi zetu?