settings icon
share icon
Swali

Kwa nini wokovu kwa kazi ni mtazamo kuu unaoshikiliwa?

Jibu


Jibu rahisi ni kwamba wokovu kwa kazi unaonekana sawa machoni pa mwanadamu. Mojawapo ya tamaa za kibinadamu ni kuwa na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, na hiyo inajumuisha hatima yake ya milele. Wokovu kwa kazi huvutia mtu na kiburi chake na tamaa ya kuwa na udhibiti. Kuokolewa kwa matendo huvutia tamaa hiyo zaidi kuliko wazo la kuokolewa kwa imani pekee. Pia, mtu ana hisia ya asili ya haki. Hata mkanamungu mwenye shauku sana anaamini aina fulani ya haki na ana hisia ya mema na mabaya, hata kama hana msingi wa maadili ya kufanya hukumu hiyo. Hisia yetu ya asili ya mema na mabaya inataka kwamba ikiwa tunapaswa kuokolewa, "kazi zetu nzuri" lazima zizidi "kazi zetu mbaya." Kwa hivyo, ni kawaida kwamba wakati mtu anajenga dini inahusisha aina fulani ya wokovu kwa kazi.

Kwa sababu wokovu kwa kazi huvutia asili ya dhambi ya binadamu, hufanya msingi wa karibu kila dini ila kwa Ukristo wa kibiblia. Mithali 14:12 inatuambia kwamba "iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti." Wokovu kwa kazi inaonekana kuwa sawa kwa wanadamu, ndiyo sababu ni mtazamo kuu unaoshikiliwa sana. Hiyo ndio haswa kwa nini Ukristo wa kibiblia ni tofauti na dini nyingine zote — ni dini pekee inayofundisha wokovu ni zawadi ya Mungu na si ya kazi. "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya Imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu" (Waefeso 2:8-9).

Sababu nyingine kwa nini wokovu kwa kazi ni mtazamo kuu unaoshikiliwa zaidi ni kwamba ni asili au kukosa wongofu wa mtu hajui kikamilifu kiwango cha dhambi yake mwenyewe au utakatifu wa Mungu. Moyo wa mwanadamu ni "mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha" (Yeremia 17:9), na Mungu ni mtakatifu kabisa (Isaya 6:3). Udanganyifu wa mioyo yetu ndiyo jambo ambalo hupotosha mtazamo wetu juu ya kiwango cha udanganyifu huo na ndicho kinatuzuia kuona hali yetu ya kweli mbele ya Mungu ambaye utakatifu wake pia hatuwezi kuelewa kikamilifu. Lakini ukweli unabakia kuwa dhambi zetu na utakatifu wa Mungu huchanganya na kufanya jitihada zetu bora kama "vitambara vichafu" mbele ya Mungu Mtakatifu (Isaya 64:6, tazama 6:1-5).

Wazo la kuwa matendo mema ya mwanadamu yangeweza kusawazisha kazi zake mbaya ni dhana isiyo ya kibiblia kabisa. Si hiyo tu, lakini Biblia pia inafundisha kwamba kiwango cha Mungu sio chini ya asilimia 100 ukamilifu. Ikiwa tunajikwaa katika kushika sehemu moja tu ya sheria ya haki ya Mungu, sisi ni wenye hatia kama tuliovunja zote (Yakobo 2:10). Kwa hivyo, hakuna njia tunayoweza kuokolewa ikiwa wokovu kwa kweli unategemea kazi.

Sababu nyingine kwamba wokovu kwa kazi inaweza kuingia polepole katika madhehebu ambayo yanadai kuwa Wakristo au wanasema wanaamini katika Biblia ni kwamba wanaelewa vibaya vifungu kama Yakobo 2:24: "Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa na haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake." Inachukuliwa katika muktadha wa kifungu kinzima (Yakobo 2:14-26), inakuwa dhahiri kwamba Yakobo hasemi kazi zetu zitatufanya kuwa wenye haki mbele za Mungu; badala yake, anafanya wazi kuwa imani halisi ya kuokoa inaonyeshwa na matendo mema. Mtu anayedai kuwa Mkristo lakini anaishi kutomtii kwa makusudi Kristo ana imani ya uongo au "iliyokufa" na hajaokolewa. Yakobo anafanya tofauti kati ya aina mbili za imani-imani ya kweli inayookoa na imani ya uongo ambayo imekufa.

Kuna mistari mingi sana ambayo inafundisha kwamba mtu haokolewi kwa kazi kwa Mkristo yeyote kuamini vinginevyo. Tito 3:4-5 ni mojawapo ya vifungu vingi hivi: "Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa mwanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu." Kazi njema hazichangii kwa wokovu, lakini daima zitakuwa tabia ya mtu aliyezaliwa tena. Kazi njema sio sababu ya wokovu; bali ni ushahidi wake.

Wakati wokovu kwa kazi inaweza kuwa mtazamo kuu unaoshikiliwa sana, sio sahihi kibiblia. Biblia ina ushahidi mwingi wa wokovu kwa neema peke yake, kupitia imani peke yake, katika Kristo peke yake (Waefeso 2:8-9).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini wokovu kwa kazi ni mtazamo kuu unaoshikiliwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries