settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa wote wemetenda dhambi?

Jibu


Usemi huu, “wote wametenda dhambi,” unapatikana katika Warumi 3:23 (“Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”) na katika kifungu cha mwisho cha Warumi 5:12 (“…kwa sababu wote wamefanya dhambi”). Kimsingi, inamaanisha kwamba sisi sote ni wahalifu , kwa sababu dhambi ni uvunjaji wa sheria ya Mungu (1 Yohana 3:4). Hali dhambi ni tabia ya maumbile ya mwanadamu; sisi sote tuna hatia mbele za Mungu. Sisi ni wenye dhambi kwa asili na kwa matendo yetu wenyewe ya uasi.

Katika Warumi 5:12 uhakika wa “wote wamefanya dhambi” inaonekana kuwa wanadamu wote “wanashiriki” katika dhambi ya Adamu na walihukumiwa kifo hata kabla ya wao wenyewe kuchagua dhambi kwa makusudi; kwa hakika, hivyo ndivyo Paulo anathibitisha katika Warumi 5:14. Ndani ya kifungu hiki (Warumi 5:12-21), Paulo anaeleza jinsi na kwa nini “hukumu ya kifo” kwa dhambi ya Adamu imewajia wanadamu wote.

Augustine alieleza upitishaji wa dhambi ya Adamu hadi kwetu kwa nadharia inayojulikana kuwa “ukuu wa shirikisho/Federal headship,” mtazamo unaoshikiliwa na wachanganuzi wengi wa kiinjilisti. Augustine alifundisha dhana ya “hatia iliyorithiwa,” kwamba sisi sote tulitenda dhambi “katika Adamu”: wakati Adamu “alipoichagua” dhambi, alitenda kama mwakilishi wetu. Kwa hivyo dhambi yake ilihesabiwa kwa kisazi chote cha mwanadamu- sote tulitangazwa kuwa na “hatia” kwa ajili ya dhambi moja ya Adamu.

Mtazamo mwingine ni kwamba usemi “wote wametenda dhambi” unarejelea tu dhambi ya kibinafsi inayotokana na asili yetu ya dhambi. Baada ya kufafanua katika Warumi 5:13-17 jinsi dhambi ya kibinafsi inavyohesabiwa na kisha kuenea, Paulo anaeleza ni kwa nini “wote wanakufa,” hata kama hawajatenda dhambi ya kibinafsi. Sababu ya wote kupokea “hukumu hii ya kifo” (Warumi 5:18a) ni kwamba, kwa kuasi kwa Adamu, wote “walifanywa kuwa wenye dhambi” (Warumi 5:19a). Kitenzi kufanyika kinamaanisha “kuundwa”; kwa hivyo, asili ya dhambi ni hali ya kurithi ambayo inaleta hukumu ya kifo, hata kwa wale ambao bado hawana hatia ya dhambi ya kibinafsi (Warumi 5:13-14). Hali ya kurithi bila kuepukika huzaa dhambi ya kibinafsi wakati dhamiri inakomaa na kumuwajibisha mtu mara tu anapoamua kuvunja sheria kimakusidi (Warumi 2:14-15; 3:20; 5:20a).

Sisi sote ni wetenda dhambi kwa sababu Adamu alipitisha hali yake ya dhambi inayoongoza bila kuepukika kwenye dhambi na kifo chetu. Watu wote hushiriki hukumu ya kifo cha Adamu kama hali ya kurithi (“asili ya dhambi”) ambayo hupitishwa na kupitia kwa wanadamu na ambayo kila mtoto huleta ulimwenguni. Hata kabla mtoto hajawajibishwa kwa ajili ya dhambi ya kibinafsi, kwa kwaida ana mwelekeo wa kuasi, kusema uwongo, nk. Kila mtoto hauzaliwa na asili ya dhambi.

“Bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu” (Zaburi 14:2). Na Mungu mwenye kuona yote anaona nini akichungulia chini? “Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja” (aya ya 3). Kwa maneno mengine, wote wametenda dhambi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa wote wemetenda dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries