settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu kukula chakula kisichofaa?

Jibu


Chakula kisichofaa ambacho ni kitamu! Kwa watu wengi, vibanzi,soda, peremende na keki ni vikundi vinne vya vyakula vya msingi. Vyakula hivi ovyo hushibisha lakini huchangia kidogo katika afya ya miili yetu. Vyakula hivi visivyofaa vimejawa na sodiamu, sukari, na mafuta. Ulaji usiosita wa vyaakula hivi unaweza kuchangia katika magonjwa ya moyo na ini na vilevile ugonjwa wa sukari. Kwa hivyo sio bora kwa afya, lakini kukula visivyofaa ni makosa? Je, Biblia inataja jambo hilo?

Mungu alipounda taifa la Israeli kama taifa kwa ajili Yake mwenyewe, aliwapa seti ya kina ya sheria ambazo walipaswa kutii (Kumbukumbu 4:1-2). Sheria hizo zilipaswa kuwasaidia kuwatenga kama taifa takatifu na kwa manufaa yao mwenyewe. Kabla ya sayansi ya lishe kugundua sababu hizo, Mungu tayari alikuwa wamewapa watu wake sheria za lishe zilizokusudiwa kuwapa afya njema (Walawi 11). Kuzingatia sheria hizo ilikua mojawapo ya sababu ambayo Mungu aliweza kuahidi Israeli kwamba hawangeteseka kutokana na magonjwa ambayo Mungu alileta juu ya Misri (Kutoka 15:26). Kwa kufuata sheria ya lishe, wangekuwa na hatari ndogo ya vimelea vya matumbo, utapiamlo na magonjwa yanayoletwa na tabia ya kula lishe isiyo bora.

Hii haimaanishi kuwa Mungu anapinga kabisa vyakula visivyo na lishe. Kwa kweli anatuhimiza kuzifurahia kama zawadi kutoka kwake. Zaburi 104 inamsifu Mungu kwa kutengeneza “divai ya kuufurahisha moyo.” Nehemia 8:10 inaagiza Israeli kusherehekea siku takatifu kwa “chakula kizuri na vinywaji vitamu.”

Huenda Maandiko ya Warumi 14:20 yakatupa mwongozo ulio wazi zaidi kuhusu chakula: “Hakika vyakula vyote ni safi, lakini ni kosa kula kitu chochote kinachomsababisha ndugu yako ajikwae.” Ingawa hii iliandikwa kwa muktadha wa ulaji wa vyakula vilivyopigwa marufuku na sheria, inaweza kuhisisha chakula ambacho sio lishe bora. Vyakula viisivyona lishe sio dhambi, lakini tukila kama walafi (Mithali 23:20) au walevi (Mithali 20:1) au tunatumia miili yetu vibaya kwa kivila, basi ulaji huo ni makosa.

Uraibu wa sukari na dawa inayopatikaka katika buni ni halisi na unaweza kuchangia maisha yasikuwa na afya nzuri kwa ujumla. Viwango vya juu vya sodiamu vilivyomo katika vyakula ovyo ni mbaya. Mungu aliumba miili yetu kuwa hekalu ya Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 3:16; 6:19-20). Tnapotumia miili yetu vibaya kupitia usafi duni, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, kujiumiza, au uraibu wa vyakula ovyo, basi hatulitunzi vyema hekalu Lake. Kula vyakula ovyo sio dhambi lakini tunavyozidi kuvikula na kudhuru miili yetu, akaunti zetu za benki, na ushuhuda wetu, basi vinaweza kuwa sanamu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu kukula chakula kisichofaa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries