Swali
Je, unao msamaha wa dhambi? Nawezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?
Jibu
Matendo 13:38 yasema, “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka nyinyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu ” (KCV).
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
Neno “kusamehe” lahusu kuchukua hatua ya kutupilia mbali makwazo ya nyuma na kuanza upya, kuwia radhi, au kufuta deni linalodaiwa. Pale tunapo mkosea mtu, huwa tunatafuta msamaha kutoka kwao ili uhusiano wetu naye urudi kuwa mzuri. Mtu hapewi msamaha kwa sababu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia majungu yoyote juu ya mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
Bibilia inatuambia ya kwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi” (TMP) . 1 Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu” (TMP). Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46; Yohana 3:36).
Msamaha - Je, mimi naupataje?
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye utayari wa kutusamehe dhambi zetu! 2 Petro 3:9 yatuambia, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (TMP). Mungu anatamani kutusamehe, hivyo ameandaa njia ili tupate msamaha.
Adhabu ya haki pekee tunayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Warumi 6:23a yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti...” (TMP), Mauti ya milele ndicho tulichojipatia kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, katika mpango wake mkamilifu, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba na kuichukua ile adhabu tuliyo stahili-yaani mauti. 2 Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye” (TMP). Yesu alikufa msalabani, akachukua adhabu ambayo sisi tulistahili! Na kwasabu Yesu ni Mungu, kifo chake kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu wote. 1 Yohana 2:2 yasema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” (TMP). Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi Wake juu ya dhambi na mauti (1 Wakorintho 15:1-28). Na Mungu asifiwe, kwani kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Warumi 6:23b yathibitika kwa kusema, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (TMP).
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, nafsi yako yakuhukumu juu ya uasi wako na hata ukijitahidi, hainyamazi? Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso 1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (TMP). Yesu alilipa deni letu ili tukapate kusamehewa. Unacho takiwa kufanya ni kumwomba Mungu akusamehe kupitia Yesu, huku ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina ujumbe huu wa kustaajabisha, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye” (TMP).
Msamaha - Kweli ni jambo rahisi namna hii?
Ndio, msamaha wapatikana kiurahisi namna hiyo! Hukuna lolote uwezalo kufanya ili ustahili msamaha toka kwa Mungu. Hauwezi kumhonga Mungu ili akusamehe. Msamaha ni wa kupokelewa tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kuomba ombi hili au ombi lingine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni katika kumwamini Yesu Kristo pekee ndipo utakapopata msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia nyepesi ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo ameichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu, na msamaha! Amina.”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
English
Je, unao msamaha wa dhambi? Nawezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?