settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kuenenda sawa na Mungu?

Jibu


Ili tuweze “kwenenda sawa” na Mungu, ni sharti tutatumbue ni sehemu gani ambapo “hatuenendi sawa” naye. Jibu la hilo ni dhambi. “Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la! hata mmoja” (Zaburi 14:3, TMP). Sote tumemuasi Mungu kwa kukeuka amri zake; Tumekuwa “tumepotea kama kondoo” (Isaya 53:6, BHN).

Habari mbaya ni kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. “Roho ile itendayo dhambi itakufa” (Ezekieli 18:4, TMP). Lakini habari njema ni kuwa Mungu mwenye upendo alitutafuta ili atuletee wokovu. Yesu alitangaza ya kwamba kusudi lake lilikuwa ni “kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10, TMP), na akakiri kukamilika kwa kusudi hilo, pale alipokufa msalabani, kwa neno “imekwisha” (Yohana 19:30, TMP).

Kuwa na uhusiano wa sawa na Mungu yaanza kwa kutambua dhambi yako. Halafu ifuate hali ya kukiri dhambi hiyo mbele za Mungu kwa kunyenyekea (Isaya 57:15, TMP). “Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu” (Warumi 10:10, KCV).

Toba hii ni sharti iambatane na imani-tukimaanisha, imani yakuwa kifo cha Yesu cha kujitoa na ufufuo wake wa kimuujiza inamwidhinisha Yeye kuwa mwokozi wako. “Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9, TMP). Vipengele vingi kwenye Biblia vinazungumzia umuhimu wa imani, kama vile Yohana 20:27; Matendo 16:31; Wagalatia 2:16; 3:11, 26; na Waefeso 2:8.

Kuenenda sawa na Mungu ni jinsi utakavyo itikia kwa kile ambacho Mungu ametenda kwa niaba yako. Alituma mkombozi, Alitoa dhabihu ya ondoleo la dhambi yako (Yohana 1:29), na anakupa ahadi kwamba: “Na itakuwa kila atakaye liita jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21, TMP).

Picha nzuri kuhusu toba na msamaha yaonekana katika ule mfano wa mwana mpotevu (Luka 15:11-32). Mwana huyo mdogo alitapanya urithi aliopewa na babake katika dhambi za kuaibisha (aya13). Alipotambua makosa yake, aliamua kurudi nyumbani (aya18). Alidhani hangeliweza kuhesabika tena kama mwana (aya19), lakini haikuwa kweli. Babae alimpenda sana huyu mwanae mwasi aliporudi, zaidi hata kuliko mwanzo (aya20), yote yalisamehewa na sherehe ikafuata (aya24). Mungu ni mwema kwa kutimiza ahadi zake, hata kwa ahadi ya msamaha. “BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo na huwaokoa waliopondeka roho” (Zaburi 34:18, KCV).

Kama unataka kuenenda sawa na Mungu, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka yakwamba, kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kuenenda sawa na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries