settings icon
share icon
Swali

Furaha ya Bwana ni nini?

Jibu


Furaha ya Bwana ni tapasamu ya moyo inayotokana na kumjua Mungu, kukaa ndani ya Kristo, na kujazwa na Roho Mtakatifu.

Wakati Yesu alizaliwa, malaika walitangaza “habari njema za furaha” (Luka 2:10). Wote wanaompata Yesu wanajua, ikiwa ni pamoja na wachungaji kuhusu kuzaliwa kwake na furaha anayoleta. Hata kabla ya kuzaliwa kwake, Yesu alikuwa ameleta furaha, kama inavyothibitishwa katika wimbo wa Mariamu (Luka 1:47) na itikio la Yohana kwa kusikia sauti ya Mariamu “aliruka kwa furaha” ndani ya tumbo la mama yake (Luka 1:44).

Yesu alidhihirisha furaha katika huduma yake. Hakuwa mnyonge; badala yake maadui zake walimshutumu kwa kuwa na furaha sana wakati mwingine (Luka 7:34). Yesu alijieleza kuwa bwana arusi anayefurahia karamu ya harusi (Marko 2:18-20); “Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu” (Luka 10:21); Alizungumza juu ya “furaha yangu” (Yohana 15:11) na akaahidi kuwapa wanfunzi Wake ruzuku hiyo katika maisha yao yote (Yohana 16:24). Shangwe imedhihirishwa katika mifano mingi ya Yesu, ikiwa ni pamoja na hadithi tatu katika Luka 15, ambazo zinataja “furahini mbele ya malaika” (Luka 15:10) na tamatisho na mchungaji mwenye shangwe, mwanamke mwenye shangwe, na baba mwenye shangwe.

Nehemia aliwaambia Waisraeli waliotubu kwamba furaha ya Bwana itakuwa nguvu yao (Nehemia 8:10). Kanisa la kwanza lilikuwa na sifa ya furaha na shangwe ya Bwana (Matendo 2:46; 13:52), na “furaha katika Roho Mtakatifu” ni alama inayotofuatisha ufalme wa Mungu (Warumi 14:17). Wale ambao ni sehemu ya ufalme wanashiriki katika furaha ya ufalme.

Furaha ni sehemu ya tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23). Kwa hakika, ni wajibu wetu wa Kikristo kufurahi katika Bwana (Wafilipi 3:1; 4:4; 1 Wathesalonike 5:16). Katika Kristo, muumini “kujawa na furaha isiyooneka yenye utukufu usioelezeka” (1 Petro 1:8).

Kwa sababu ya asili yake isiyo ya kawaida, furaha ya Bwana-tabasamu yetu ya moyo- iko hata wakati tunapitia majaribu ya maisha. Tunajua sisi ni watoto wa Mungu, na hakuna mwenye anaweza kutunyakua kutoka Kwake (Yohana 10:28-29). Sisi ni warithi wa “urithi usioweza kuangamia, kuharibika au kufifia,” na hakuna awezaye kuuiba kutoka kwetu (1 Petro 1:4; Mathayo 6:20). Tunamwona Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu, na acha adui akasirike hata zaidi, tunajua ni nani atakayeshinda mwishowe (Waebrania 12:2; Zaburi 2).

Imani ndio nguzo inaoushinda ulimwengu, na furaha ya Bwana ni nguvu zetu. Hali mbaya, badala izuie imani yetu, hakika inaweza kuzidisha furaha yetu. Paulo na Sila walijua dhiki walipoketi huku miguu yao imefungwa na minyororo katika seli ya gereza ya Filipi. Haki zao za kisheria zilikuwa zimekiukwa. Walikuwa wamekamatwa bila sababu na kupigwa bila kupelekwa mahakamanii. Usiku wa manane, kwa vile hawakuweza kulala, waliimba-kwa sauti kubwa-sifa za Bwana waliokuwa wakimtumikia (Matendo 16:25). Muujiza ulifuata upesi (mstari wa 26).

Mitume huko Yerusalemu walikamatwa-mara mbili-na kuamrishwa wasihubiri katika jina la Yesu. Mara ya pili walipokabiliwa na mahakama, walipigwa. Bila kufadhaika, walirudi nyumbani “wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu” na kuwa tayari kuhubi zaidi (Matendo 5:41). Bila shaka, mitume walikuwa wakifuata tu kielelezo cha Bwana wetu, ambaye “kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba” (Waebrania 12:2).

Furaha ya Bwana inaweza kuwa isiyoelezeka kwa yule ambaye hana hiyo furaha. Lakini, kwa muumini katika Kristo, furaha ya Bwana huja kwa kawaida kama zabibu kwenye mzabibu. Tunapodumu katika Kristo, Mzabibu wa kweli, sisi ambao ni matawi, tumejawa nguvu na uchangamfu Wake, na matunda tunayozaa, ikiwa ni pamoja na furaha, yote ni kazi yake (Yohana 15:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Furaha ya Bwana ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries