settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kuandama haki?

Jibu


Mithali 15:9 inasema, “Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.” Ikiwa Mungu anatuhitaji kufuata haki, je, na vifungu kama Warumi 3:10 ambayo yasema, “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja?” Ikiwa hakuna mwenye haki, basi ni nani anayeweza kuifuata haki? Je, vifungu hivyo vinakinzana?

Kabla tuanze kutafuta uadilifu, ni lazima kuufafanua. Neno linalotafsiriwa mara nyingi “haki, uadilifu, au utakatifu wa kiungu.” Kiwango cha Mungu ndicho hufafanua uadilifu wa kweli; nguvu zake ndizo zinazowezesha. Isipokuwa Mungu awe ndiye mwanzilishi, kamwe hatuwezi kupata haki. Hakuna kiwango chochote cha juhudi za mwanadamu kitaleta uadilifu. Kuwa mwadilifu ni kuwa sawa na Mungu. Moyo ulio sawa na Mungu huleta maisha yanayozaa “matunda” (Yohana 15:1-2; Marko 4:20). Wagalatia 5:22-23 huorodhesha baadhi ya matunda hayo.

Kibadala cha kawaida cha uadilifu wa kweli ni kujihesabia haki. Kijihesabia haki ni kinyume cha kile Mungu anataka. Kujihesabia haki hutengeneza orodha ya sheria na kuzifuata, ukijipongeza kwa jinsi unavyofanya vizuri ukilinganishwa na mwingine. Mafarisayo wa siku za Yesu walikuwa mabwana wa kujiona kuwa waadilifu, lakini Yesu alikuwa na maneno makali kwao: “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo yanapendeza kwa nje, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. Vivyo hivyo, kwa nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu” (Mathayo 23:27-28).

Kuandama haki kunamaanisha kuwa ni lazima tutambue kwamba hatuwezi kumpendeza Mungu katika hali yetu ya dhambi (Warumi 8:8). Tunageuka kutoka kujaribu kujihesabia haki kwa matendo yetu mema na badala yake kutafuta rehema ya Mungu. Tunatamani kwamba abadilishe akili zetu (Warumi 12:2) na atufananishe na “mfano wa Mwanawe” (Warumi 8:29). Katika Agano la Kale, wanadamu walitangazwa kuwa wenye haki walipomwamini Mungu na kuchukua hatua kwa hilo (Mwanzo 15:6; Wagalatia 3:6; Yakobo 2:23). Kabla ya Pentekoste (Matendo 2:1-4), watu walifuata haki kwa kuishika Sheria ya Mungu, kutafuta utakatifu, na “kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako” (Mika 6:8). Hakuna aliyehesabiwa haki kwa kuifuata sheria bali kwa imani iliyowawezesha kumtii Mungu (Warumi 3:20; Wagalatia 2:16).

Vile vile, leo hii tumehesabiwa haki kwa imani inayotuongoza kwa Yesu (Warumi 3:28; 5:1; 10:10). Wale walio ndani ya Kristo wanaendelea kumtafuta Mungu ili wampendeze (Wakolosai 3:1). Tunapokuja kwa imani katika Kristo, Yeye hutupa Roho Mtakatifu ambaye hutuwezesha kutaftua haki kwa ajili yake (Matendo 2:38). Anatuamuru “kuenenda katika Roho” (Wagalatia 5:16, 25). Kuenenda katika Roho inamaanisha tunaishi mtindo wa maisha ya kujisalimisha kikamilifu kwa utawala wa Yesu Kristo. Tunakuza uwezo wa kumsikia Mungu na tabia ya mazoea ya kutii sauti yake katika kila jambo.

Tunafuata haki wakati tunafuata tabia ya Kristo na kutamani utaktifu zaidi ya anasa za kimwili. Tunaepuka jaribio la kujihesabia haki tunapoelewa kwamba uadilifu wa kweli huanza na unyenyekevu wa kiungu (Zaburi 25:90). Tunakumbuka kwamba yesu alisema, “pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote” (Yohana 15:5). Wakati tunachukua muda wetu mbele za Mungu, tunakuwa na ufahamu zaidi wa dhambi zetu wenyewe na mapungufu. Fulana mbovu inaonekana nyeupe kando ya ukuta wa giza. Lakini, ikilinganishwa na theluji, shati hilo linaonekana chafu. Kiburi na kujihesabia haki haviwezi kubaki katika uwepo wa Mungu mtakatifu. Kufuatia haki huanza wakati moyo mnyenyekevu unapotatufa uwepo wa Mungu daima (Yakobo 4:10; 1 Petro 5:6). Moyo mnyenyekevu huelekeza kwenye maisha ya matendo ya haki yanayokubalika na Mungu (Zaburi 51:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kuandama haki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries