settings icon
share icon
Swali

Je, ni makosa kumlaumu Mungu? Je, kumlaumu Mungu ni dhambi?

Jibu


Kumlaumu Mungu ni jibu la kawaida wakati maisha hayaendi tunavyoyaka. Kwa kuwa Mungu ndiye anayetawala kila kitu, tunafikiri kwamba, angekomesha kilichotokea. Angeweza kubadilisha hali hiyo kunifaidi mimi; angeweza kuepusha janga hilo. Kwa kuwa hakufanya hivyo, Yeye ndiye anayelaumiwa.

Kwa maana moja, kauli hizo ni za kweli. Isaya 45:7 inaonekana kudhibitisha wazo la kwamba Mungu ndiye wa kulaumiwa kwa kila kitu kinachotokea: “Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa.Mimi, Bwana, huyatenda haya yote.” Na Isaya 46:9–11: “ Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale;mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine;mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi…. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.’..Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza; lile nililolipanga, ndilo nitakalolitenda.” Ikiwa Mungu yuko tayari kuwajibika kwa kila jambo , je ni makosa kumlaumu wakati janga au mambo ya kuvunja moyo yanapotendeka?

Neno lawama linamaanisha “kutafuta makosa.” Kulaumu kunapita zaidi kukiri enzi kuu ya Mungu. Kumlaumu Mungu inaonyesha kwamba alifanya makosa, kwamba kuna kosa ndani yake. Tunapomlaumu Mungu tunajifanya kuwa waamuzi wake. Lakini wanadamu hawana haki ya kutoa hukumu kwa Mwenyezi Mungu. Sisi ni viumbe wake; Yeye sio kiumbe wetu. “Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake, yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi. Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi, ‘Unatengeneza nini wewe?’Je, kazi yako husema,‘Hana mikono’? Ole wake amwambiaye baba yake,‘Umezaa nini?’Au kumwambia mama yake,‘Umezaa kitu gani?’” (Isaya 45:9-10).

Ili tuepuke kumlaumu Mungu, lazima kwanza tuelewe kwa nini kuvunjika moyo na uchungu ni sehemu ya maisha yetu. Ulimwengu wa dhambi. Tuliumbwa kikamilifu ili kuishi katika ulimwengu mkamilifu (Mwanzo 1-2). Lakini dhambi ya Adamu ilileta uharibifu na masaibu katika ulimwengu mkamilifu wa Mungu. Vimbuga, tufani, mtetemeko wa ardhi, ukame – hatimaye, majanga yote ya asili yapo kwa sababu ya dhambi (Mwanzo 3:17-19). Chaguzi zetu zenye dhambi huleta athari mbaya ambayo huendelea maishani yetu. Na dhambi za wengine hutuathiri sisi pia. Shida ya dunia ni kumbusho kwamba dhambi ina matokeo mabaya, kwa hivyo kabla kumlaumu Mungu kwa matatizo lazima tuchunguze maisha yetu wenyewe na kuwa waaminifu kuhusu chaguzi zetu ambazo ziliweza kusababisha matatizo hayo.

Pili, tunahitaji kuchunguza uhusiano wetu na Mungu. Inashangaza kwamba watu wengi ambao hawamfikirii Mungu kamwe wanapofanya mambo yao wenyewe wanakuwa watu wa dini wakati janga linapotokea. Asilimia 99 ya wakati wanaishi kwa ajili yao, kana kwamba hakuna Mungu. Lakini janga linapotokea, gafla inakuwa ni makosa ya Mungu. Hili sio jambo la busara na pia ni kumtusi Muumba aambaye tayari ametupa yote tunayojitaji ili kuwa na uhusioano naye.

Bila shaka, kuwa na uhusiano mzuri na Bwana haituondolei mambo ya kuvunja moyo. Je, tunafanya nini wakati janga linapotupata? Mara nyingi, wakristo wanajaribiwa kumlaumu Mungu wakati mahangaiko yanapokuja. Tuna tabia ya kufuata ushauri wa mkewe Ayubu kwa mume wake anayeteseka: “Mlaani Mungu nawe Ukafe!” (Ayubu 2:9).

Badala ya kumlaumu Mungu, Wakristo wanaweza kumkimbilia ili kupata faraja (Mithali 18:10; Zaburi 34:18). Wakristo wana ahadi ambayo wasioamini hawawezi kudai. Warumi 8:28 inasema kwamba “Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” Wengine hunukuu mstari huu na kuwacha baada ya neno mema, lakini hio ni matumizi mabaya ya Maandiko. Mungu aliweka sifa mbili zinazostahili baada ya ahadi hii ambazo zinafafanua mipaka yake:ahadi ni kwa wale “wanaompenda Mungu” na wale “walioitwa kwa kusudi lake.”

Badala ya kumlaumu Mungu, wanaompenda waweza kukabili janga wakiwa na uhakikisho kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwadhuru ambacho Mungu hakuruhusu kwa sababu nzuri na yenye upendo. Yeye huruhusu mambo magumu hata mateso na kifo, kwa makusudi Yake ya juu zaidi. Tunapotamani mapenzi ya Mungu katika maisha yetu, na kuyatanguliza kuliko mapenzi yetu, Yeye huwa hapotezi chochote. Hakuna mateso, huzuni, hasara au maumivu yanayopotezwa katika maisha ya watu wa Mungu. Yeye hubadilisha huzuni na hasara kuwa jukwaa ya huduma ya siku za usoni. Anatumia mambo magumu kutitia nguvu, na kutupa nafasi kubwa zaidi ya kuweka hazina mbinguni ambayo hatungekuwa nayo bila uchungu huo (Mathayo 6:20). Badala ya kumlaumu Mungu, “tunashukuru kwa kila jambo” (Waefeso 5:20; I Wathesalonike 5:18).

Tunakubali kwamba Mungu anaweza kuingilia kati katika hali yoyote; asipoingilia kati na msiba ukatokea, tunapaswa kuwacha kumlaumu kwa makosa. Katika mateso ya Ayubu yote, “Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya” (Ayubu 1:22). Badala ya kumlaumu Mungu, amabaye aliruhusu hasara kubwa, Ayubu alisema, “ingawa ataniua bado nitamtumaini” (Ayubu 13:15). Mungu aliheshimu jibu la Ayubu na kumbariki zaidi baada ya kupita jaribu hilo. Mungu anataka kutubarki vilevele, kwa ufahamu mkubwa, kujitolea zaidi na thawabu ya milele ambayo kamwe haiwezi kuondolewa. Tunapojaribiwa kumlaumu Mungu, tunaweza kuchagua jibu la Ayubu na kuamini kwamba anajua anachokifanya (Tazama Zaburi 131)

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makosa kumlaumu Mungu? Je, kumlaumu Mungu ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries