settings icon
share icon
Swali

Je inamaanisha nini kumpenda Mungu?

Jibu


Kwanza, kumpenda Mungu kunahitaji kumjua Yeye, na ufahamu huo unaanza na Neno Lake. Inaweza oonekana kuwa jambo rahisi, lakini kumjua ni kumpenda Yeye.

Kumpenda Mungu ni kumwabudu na kumsifu Yeye. “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake” (Luka 4:8). Kitabu cha Zaburi kinatoa mifano mingi mizuri ya jinsi ya kumwabudu na kumsifu Muumba wetu (k.m. Zaburi 8, 19, 23, 24, 67, 99, 117, na 150).

Kumpenda Mungu ni kumtanguliza kwa kila jambo. Amri ya kwanza ni kumpenda Mungu “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote” (Marko 12:30). Ni upendo usiogawanyika. Mungu ndiye kitu cha kwanza kwetu. Ikiwa tunampenda Mungu kwa mioyo yetu yote, nafsi zetu zote, akili zetu zote na nguvu zetu zote, basi hatutaruhusu mambo mengine yatuingie. Upendo wetu kwa Mungu unadhihirika katika kupenda watu (Marko 12:31), lakini hatupendi vitu vya ulimwengu. “Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe” (Zaburi 73:25). Hatuwezi kupenda ulimwengu wa sasa na Mungu kwa wakati mmoja (1 Yohana 2:15); kupenda yale ambayo ulimwengu hutoa kunaweza kutupotosha (2 Timotheo 4:10).

Kumpenda Mungu ni kumtamani, kutamani haki yake, Neno lake, na neema yake. “Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu” (Zaburi 42:1). Pindi tu tumeonja na kuona kwamba Bwana ni mwema (Zaburi 34:8), tunataka zaidi kutoka kwake. Ikiwa tunampenda Mungu, tutakuwa kama Mariamu wa Bethania, “ambaye aliketi chini miguuni mwa Bwana akisikiliza yale aliyokuwa akisema” (Luka 10:1). Ikiwa tunampenda Mungu, maelezo ya mtunga zaburi ya Neno la Mungu yatakuwa na maana kwetu: “Ni za thamani kuliko dhahabu,kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega” (Zaburi 19:10).

Sembuse mwanaume ametenganishwa na mpenzi wake na kupokea barua kutoka kwake. Hatua yake ya kwanza itakuwa kufungua ile barua kwa hamu na kuusoma ujumbe uliomo. Upendo wake kwa mpendwa wake utamfanya apende mawasiliano yake naye. Ndivyo ilivyo katika upendo wetu kwa Neno la Mungu. Kwa sababu tunampenda Mwandishi, tutapenda ujumbe wake kwetu. Tunalisoma kwa bidi na mara nyingi, tunilishikilia kwa karibu, na tunayaficha maneno yake mioyoni mwetu.

Mwisho, kumpenda Mungi ni kumtii. Yesu anatuambia “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15, 23; 15:10; 1 Yohana 5:3). Ingawa hili si suala la kufuata tu sheria na kuzalisha matendo mema. Ni kuwa na upendo wa Mungu umeandikwa bila kutufika mioyoni mwetu. Kwa kawaida tunatamani kuwafurahisha wale tunaowapenda. Tunapompenda Mungu, tutataka kumpendeza na kutii amri zake kwa hamu. ”Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako” (Zaburi 40:8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je inamaanisha nini kumpenda Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries