settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kumpendeza Mungu?

Jibu


Kumpendeza Mungu ni au kunapaswa kuwa lengo la waumini wote-wote wanaoliita jina la Kristo kwa ajili ya wokovu. Vinavyohitajika kwa wale wote wanaotaka kumpendeza Mungu ni kwamba ni lazima wamtafute Mungu kwa imani, watembee katika Roho na sio katika mwili, na mwenendo unaostahili wito wao katika utiivu na kunyenyekea kwa mapenzi ya Mungu. Mambo haya yanaweza kuonekana yasiowezekana kufanya, lakini Mungu anatutaka tumpendeze Yeye, na anaifanya rahisi kumpendeza Yeye. Tunafanya mambo haya kwa nguvu ya Roho Wake anayeishi mioyoni mwetu.

Paulo anawakumbusha waumini wa Rumi kwamba “wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:8). Kwa hivyo hatua ya kwanza katika kumpendeza Mungu ni kukubali dhabihu ya dhambi ambayo aliitoa katika kifo cha Kristo msalabani. Ni hapo pekee sisi tulio “katika Roho” na sio “katika mwili.” tunafanya hivyo kwa imani kwa sababu “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidi” (Waebrania 11:6).

Katika Warumi 8, Paulo anaeleza tofauti kati ya asili ya dhambi na asili ya wale waliofanywa upya na Roho. Wale ambao bado wako katika dhambi zao huwa na mawazo yao juu ya tamaa za dhambi, ambapo wale waliozaliwa upya na Kristo wana akili mpya kabisa ambayo inatawaliwa na Roho na kutamani kuishi kulingana naye. “Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:6-7). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa waumini katika kumpendeza Mungu ni kuwa na uhakika kwamba tunaenenda katika Roho, si katika mwili.

Zaidi ya hayo, ni lazima tuishi kwa imani (Waebrania 10:38). Mungu hawezi kupendezwa na wale “wanaorudi nyuma” kutoka kwake kwa sababu hawana imani Naye au wana shaka na matamko ya ukweli na ahadi Zake, au ambao hawaamini kwamba njia Zake ni sawa na takatifu na kamilifu. Sharti la imani na ujasiri katika Mungu sio kitu kisicho na maana; ni kile tunachohitaji kwa watoto na wenzi wetu, ni hali ya lazima ya kuwa radhi nao. Ndivyo ilivyo kwa Mungu.

Kwa hivyo, kumpendeza Mungu ni suala la kuishi kulingana na maagizo, amri zake, na kufanya hivyo kwa upendo. Mara nyingi tunataka kuwafurahisha wale tunaowapenda, na Agano Jipya limejaa mawaidha ya kuishi maisha ya haki na kumpendeza Kristo kwa kutii amri zake. Yesu aliliweka hili wazi kabisa: “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15). Nyaraka ni mpango wa Mungu kwa waumini na zimejawa na mawaidha ya kuyadhihirisha katika maisha yetu yote na tabia ambayo ni ya kumpendeza Mungu: “Hatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Yesu kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo” (1 Wathesalonike 4:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kumpendeza Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries