settings icon
share icon
Swali

Je, ufunguo gani kwa ushindi katika kushindana na dhambi?

Jibu


Kuu zaidi kwa ushindi wetu katika mapambano na dhambi halipo ndani yetu wenyewe, bali katika Mungu na uaminifu wake kwetu: “Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu” (Zaburi 145:18; ona pia Zaburi 46:1).

Hakuna njia ya mkato: sisi wote hupambana na dhambi (Warumi 3:23). Hata mtume mkuu Paulo aliomboleza juu ya mapambano yake yaliyoendelea na dhambi katika maisha yake: “Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu” (Warumi 7:18-20). Pambano la Paulo na dhambi lillikuwa la kweli; hata akapaza sauti, “Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” (Warumi 7:24)

Bali katika andiko linalofuata, anajibu swali lake mwenyewe, na pia swali letu: “Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 7:25). Katika kifungu hiki, Paulo hatupi ufunguo hasa wa ushindi tunapopambana na dhambi, bali anaeleza utata usioisha kati ya asili yetu ya dhambi na asili ya kiroho: “Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi” (Warumi 7:25).

Mbeleni Paulo alisema, “Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi” (Warumi 7:14). Paulo analinganisha asili yetu ya dhambi, mwili wetu, na mtumwa. Kama vile mtumwa anavyomtii bwana wake, vivyo hivyo mwili wetu hutii dhambi. Ingawa, sisi waumini katika Kristo, tumekuwa viumbe wa kiroho chini ya sheria ya Kristo; nafsi zetu za ndani ziko chini ya ushawishi na umiliki wa neema ya Mungu na uzima wa Kristo (Warumi 5:21). Maadamu tunaishi katika ulimwengu huu, asili yetu ya dhambi na tamaa ya kimwili itabaki kwetu. Lakini pia tuna asili mpya katika Kristo. Hili huleta pambano kati ya kile tunachotaka kufanya na kile tunachofanya hasa, huku dhambi ikiendlea kushambulia asili yetu ya kidunia. Mapambano haya ni sehemu ya kawaida ya kuishi maisha ya Kikristo.

Inafurahisha kuona kwamba Paulo, mtume mkuu zaidi, alitangaza kwamba, kati ya wenye dhambi wote, “mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote” (1 Timotheo 1:15). Paulo anathibitisha mapambano sisi sote tunapopigana na dhambi na majaribu katika maisha yetu. Mapambano ni ya kweli, na yanadhoofisha. Tunachoka kutokana na majaribu yasiyoisha na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Paulo kimsingi, anatuambia kwamba hatuhitaji kujifanya kuwa hatujaguswa na mapambano yetu. Amewahi pitia. Anaelewa zaidi. Ijapokuwa juhudi zetu za kufanya mema zinapoonekana kufifia, tunalo tumaini “kupitia Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 7:25; Waebrania 4:15). Na hakika Yeye ni ufunguo wa ushindi wetu dhidi ya dhambi.

Mkristo wa kweli atapigana na Shetani na jitihada zake za kila siku za kutudhoofisha. Ibilisi ndiye mtawala wa ulimwengu huu, na tunaishi “nyuma ya mipaka ya adui” (Waefeso 2:2; 6:12; Yohana 12:31). Tukimtazamia Kristo, hata hivyo, tutaweza kusitawisha mtazamo unaotangaza kwamba tungependa kufa kuliko kufanya lolote la kumuudhi Mungu. Wakati tunajitoa kwa Kristo kabisa (Mathayo 16:24), Shetani atatukimbia. Tunapomkaribia Mungu, Yeye naye atatukaribia (Yakobo 4:7-8).

Ufunguo wetu wa ushindi katika mapambano yetu na dhambi upo katika ahadi ya Mungu Mwenyewe: “Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili” (1 Wakorintho 10:13).

Kama waumini wa kweli katika Kristo, hata watakati “tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia” (2 Wakorintho 1:8), tunaweza kuangwi maneno yenye ya uhakikisho ya Paulo, ambaye anatangaza, “Yeye aliyetuokoa kwenye hatari kubwa ya kifo na atatuokoa tena” (1 Wakorintho 1:10). Mwisho, mtunga zaburi anatupa maneno ya kutia moyo: “Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako. Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili” (Zaburi 37:3-5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ufunguo gani kwa ushindi katika kushindana na dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries