settings icon
share icon
Swali

Je, inawezekana kuwa mtakatifu, kwa vile ni Mungu pekee ndiye mtakatifu?

Jibu


Utakatifu sio tu uwezekano kwa Mkristo; utakatifu ni hitaji. “Na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” (Waebrania 12: 14). Tofauti kati ya Mungu na sisi ni kwamba Yeye kwa asili ni mtakatifu huku sisi, kwa upande mwingine, tunakuwa watakatifu katika uhusiano kwa Kristo pekee na tunaongezeka katika utakatifu wa vitendo tunavyokomaa kiroho. Agano Jipya linasisitiza masumbuo ya utakatifu katika huu ulimwengu na mafanikio ya mwisho ya utakatifu katika ulimwengu utakaokujaf

Kuwa “mtakatifu” inamaanisha kwamba sisi, kwanza kabisa, “tumetengwa kwa matumizi ya heshima”. Kumbe tulikuwa “hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumia tamaa na anasa za namna nyingi … Mwokozi wetu Mungu … alituokoa, si kwa sababu ya matendo yahaki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu” (Tito3:3-5; cf. 1 Wakorintho 6:11). Bwana alichukua mpango wa kututoa katika mitindo yetu ya maisha ya awali. Alituokoa, alitutakasa, na kututenga kwa haki. Ikiwa tumeaamini katika Kristo kwa wokovu, tumeoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na Roho Mtakatifu na kutengwa kutoka kwa ulimwengu kwa utauwa (ona Warumi 12:2).

Hata hivyo, kutafuta utakatifu hakuishi tunapokuja kwa Kristo. Kwa kweli, inaanza! Kuna utakatifu wa nafasi ambao tunarithi katika kuzaliwa kwa pili na utakatifu wa vitendo ambao lazima tutafute vikamilifu. Mungu anatarajia tukuze mtindo wa maisha wenye utakatifu (1Petro 1:14-16) na kutuamru “tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu” (2 Wakorintho 7:1). Kuleta utakatifu kwa “ukamilifu” inamaanisha kwamba tunapaswa kuongezeka katika matunda ya kiroho kila siku. Tunahitaji kuzingatia sisi wenyewe “wafu kwa dhambi” (Warumi 6:11),na kukataa kurudi nyuma katika mitindo ya maisha yetu ya awali. Kwa njia hii “kujitakasa kutoka kwa kile kisicho na heshima,” atakuwa chombo cha kupata “heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana …. Kwa kila kazi iliyo njema” (2Timotheo 2:21). Utakatifu ni alama ya kila Mkristo wa kweli (1 Yohana 3:9-10).

Kukuza mtindo wa maisha ya utakatifu haimaanishi kwamba lazima tuandike orodha ya kufuata ya cha kufanya na ambacho hufai kufanya. Tuko huru kutoka kwa barua ya sheria ambayo inaua (2 Wakorintho 3:6) na sasa ishi kulingana na amri ya Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:16-18).

Tunaambiwa, “Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema” (Wafilipi 2:12-13). Katika mstari huu, tunaona ushirikiano kati ya Mungu na watoto Wake katika utakaso. “Tunafanya” kile Mungu “anafanya” ndani yetu, kwa sababu Mungu ana ratiba ya wema ambao anapendelea kukuza katika maisha yetu. Wajibu wetu ni kutii matamanio Yake, “kufanya” kwa umakini na utunzaji mkubwa kwa vile vitu ambazo Yeye anafanya kukua ndani yetu. Utakatifu hauwezi kuletwa kwa ukamilishaji katika maisha yetu bila juhudi kwa upande wetu. Tumealikwa kushiriki katika kazi ya Mungu ndani yetu. Hatuwezi “bebwa kuenda kwa anga katika kitanda chenye maua ya raha,” vile wimbo wa zamani wa kidini unavyosema.

Hii, pengine, ni somo muhimu zaidi tunaweza jifunza kama Wakristo. Mapenzi kuu ya Mungu kwa watu Wake ni kwamba tuwe watakatifu—kuendana katika mfano wa Mwana Wake, Yesu (Warumi 8:29; 1 Wathesalonike 4:3-4). Utakatifu ni matakwa ya Mungu kwa maisha yetu.

Bila haka, mwili ni dhaifu (Marko 14:38). Hakuna mwenye atafikia ukamilifu usio na dhambi katika ulimwengu huu, lakini Mungu amefanya maandalizi kwa dhambi zetu. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Kutafuta kwetu kwa utakatifu katika ulimwengu huu kunajumuhisha kukiri na kuacha dhambi kila siku (ona Waebrania 12:1-3).

Mungu anatusaidia katika udhaifu wetu kwa kutupatia Roho Mtakatifu ambaye hutufunulia nia ya Kristo kwetu na anatuwezesha kutekeleza matakwa Yake (Wakorintho 2:14-16; Wafilipi 2:13). Wakati tunatii Roho, tunakuwa Wakristo wenye kuzaa matunda, tukizaa mavuno yanayompendeza Mungu (Wagalatia 5:22-23). Kwa upande mwingine, tunapokandamiza kazi ya Roho Mtakatifu kwa kuasi matakwa Yake kwetu, tunakandamiza mpango wa Mungu, tunaharibu ukuaji wetu wenyewe wa kiriho, na kuzunisha Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30).

Ikiwa Mungu alikuwa na fadhili ya kutosha kutukomboa kutoka kwa dhambi na kifo na kutupa maisha mapya katika Kristo, cha msingi tunaweza kufanya ni kutoa maisha yetu Kwake katika kujikabidhi vikamilifu na utakatifu, ambayo ni kwa faida yetu (cf Kumbukumbu la Torati 10:13). Kwa sababu ya huruma ya Mungu, tunahitaji kuwa dhabihu lililohai, “takatifu, ya kumpendeza Mungu” (Warumi 12:1; cf. Kumbukumbu la Torati 10:13). Siku moja, mbinguni, tutakuwa huru kutoka kwa dhambi na madhara yake yote. Hadi wakati huo, “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu” na kuendelea kukimbia mbio zetu (Waebrania 12:2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inawezekana kuwa mtakatifu, kwa vile ni Mungu pekee ndiye mtakatifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries