settings icon
share icon
Swali

Nguzo kuu ya kuzaa matunda kama Mkristo ni gani?

Jibu


Katika ulimwengu wa asili, matunda ni matokeo ya mmea wenye afya unaozalisha kile ulichoundwa kuzalisha (Mwanzo 1:11-12). Katika Biblia, neno tunda limetumika mara nyingi hutumiwa kufafanua matendo ya nje ya mtu yanayotokana na hali ya moyo.

Tunda zuri ni lile limezalishwa na Roho Mtakatifu. Wagalatia 5:22-23 inatupa mahali pa kuanzia: Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Kadri tunavyomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze maishani mwetu, ndivyo tunda hili linaonekana zaidi (Wagalatia 5:16, 25). Yesu aliwaambia wafuasi wake, “bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu” (Yohana 15:16). Matunda ya haki yana faida ya milele.

Yesu alituambia waziwazi kile tunachopaswa kufanya ili kuzaa matunda mazuri. Alisema, “Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda. “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote” (Yohana 15:4-5). Tawi lazima likae imara kwenye shina ili libaki kuwa hai. Kama wanafunzi wa Kristo, ni lazima tuendelee kushikamana Naye kwa uthabiti ili tuendelee kuzaa matunda ya kiroho. Tawi linatoa nguvu , lishe, ulinzi, na nishati kutoka kwa mzabibu. Ikiwa limevunjwa, litakufa haraka na linakuwa lisilozaa. Tunapopuuza maisha yetu ya kiroho, kupuuza Neno la Mungu, kuomba nadra sana, na kuzuia sehemu za maisha yetu kutoka kwa uchunguzi wa Roho Mtakatifu, tunakuwa kama tawi lililokatwa kutoka kwa mzabibu. Maisha yetu yanakuwa hayana matunda. Tunahitaji kujisalimisha kila siku, mawasiliano ya kila siku, na kila siku-wakati fulani kwa sasa-toba na kuunganishwa na Roho Mtaktifu ili “twenende kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili” (Wagalatia 5:16). Kukaa kwa uhusiano wa karibu na Mzabibu wa kweli ndiyo njia pekee ya “kuzaa matunda hata wakati wa uzee ” (Zaburi 92:14), na “kupiga mbio wala hawatachoka” (Isaya 40:31), na “kutochoka kutenda mema” (Wagalatia 6:9).

Pingamizi moja kwa kuzaa matunda ni unafiki. Tunakuwa wataalamu katika utaratibu, lugha, na “kuonekana kama Wakristo,” huku tukiwa hatuna uzoefu wowote wa nguvu halisi na kukosa kuzaa matunda. Mioyo yetu inabaki ikiwa na ubinafsi, hamaki, na bila furaha hata wakati tunapitia katika hali ya kumtumikia Mungu. Kwa urahisi sana tunaweza kuteleza kwa dhambi ya Mafarisayo wa siku za Yesu katika kujihukumu sisi wenye jinsi tunavyofikiri tunaonekana kwa wengine na kupuuza mahali pa siri pa moyo ambapo matunda mema yote huchibuka. Wakati tunapenda, tamani, tafuta na kuogopa kitu kile kile ambacho ulimwengu wote unaogopa, hatukai ndani ya Kristo, hata kama maisha yetu yemejawa na shughuli za kanisa. Na, mara nyingi, hatutambui kwamba tunaishi maisha yasiyo na matunda (1 Yohana 2:15-17).

Kazi zetu zitajaribiwa kwa moto. Kwa kutumia sitiari tofauti na matunda, 1 Wakorintho 3:12-15, inasema, ”Kama mtu yeyote akijenga juu ya msingi huu kwa kutumia dhahabu, fedha, vito vya thamani, miti, majani au nyasi, kazi yake itaonekana ilivyo, kwa kuwa siku ile itaidhihirisha. Itadhihirishwa kwa moto, nao moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu yake. Kama kazi kitateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini tu kama mtu aliyenusurika kwenye moto.”

Mungu ndiye mwamuzi wa hata mawazo na misukumo yetu. Yote yataletwa kwenye nuru tutakaposimama mbele zake (Waebrania 4:12-13). Mjane maskini katika chumba kimoja anaweza kuzaa matunda mengi kama vile mwinjilisti wa runinga anayeongoza mikutano mikubwa ya msalaba ikiwa amejisalimisha kwa Mungu katika kila kitu na kutumia yote ambayo Amempa kwa utukufu Wake. Kwa vile matunda ni ya kipekee kwa kila mti, tunda letu ni la kipekee kwetu. Mungu anajua kile ambacho amemkabidhi kila mmoja wetu na kile anachotarajia tufanye nacho (Luka 12:48). Wajibu wetu mbele za Mungu ni kuwa “mwaminifu na vichache” ndipo aweze kutuamini na vingi (Mathayo 25:21).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nguzo kuu ya kuzaa matunda kama Mkristo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries