settings icon
share icon
Swali

Je, ina maanisha nini kuwa mkristo aliye zaliwa mara ya pili?

Jibu


Je ina maanisha nini kuwa mkristo aliye zaliwa mara ya pili? Sehemu kamilifu katika Bibilia inayo jibu swali hili ni Yohana 3:1-21. Bwana Yesu Kristo akizungumza na Nikodemo, aliyekuwa mfarisayo wa kuheshimika na mmoja wa Baraza kuu la Wayahudi (yaani Sanhedrini). Nikodemo alimjia Yesu usiku akiwa na maswali ya kumuuliza.

Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, “Amin, Amin, nakuambia: mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia: Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, ‘Hamna budi kuzaliwa mara ya pili…’ (Yohana 3:3-7, TMP).

Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “kuzaliwa toka juu” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kiroho. Kuzaliwa upya, yaani kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2 Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1 Petro 1:3; 1 Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana 1:12, 13 yaonyesha kuwa ”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika watoto wa Mungu” pale tuwekapo imani yetu katika jina la Yesu Kristo.

Sasa swali lafuata, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu” (KCV). Kwa Warumi, aliwaandikia katika Warumi 3:23 akisema..., ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (TMP). Wenye dhambi ni wafu “kiroho”, lakini pale wanapopokea uzima rohoni kwa kumwamini Kristo, hapo ndipo Biblia hulinganisha jambo hilo na kuzaliwa mara ya pili. Wale tu waliozaliwa mara ya pili ndio wenye msamaha wa dhambi na uhusiano na Mungu.

Je, hii hutokea vipi? Waefeso 2:8-9 yasema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu awaye yote asije akajisifu” (KCV). Mtu anapo “okolewa”, basi yeye amezaliwa mara ya pili, afanywa upya kiroho, na kufanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya sisi “kuzaliwa mara ya pili” kiroho. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya.” (2 Wakorintho 5:17, TMP).

Kama bado hujawahi kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kumsikiliza Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, utaomba maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13, TMP).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba, kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ina maanisha nini kuwa mkristo aliye zaliwa mara ya pili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries