settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kumkubali Yesu kama Mwokozi wako binafsi?

Jibu


Je, umeshawahi kumkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wako binafsi? Ili kulielewa hili swali, ni sharti kwanza kuelewa maana ya 'Yesu Kristo', 'Mwokozi' na 'Binafsi.'

Kwanza, Yesu Kristo ni nani? Watu wengi wanamtambua Yesu Kristo kama mtu mwema, mwalimu mashuhuri, au hata nabii wa Mungu. Haya maelezo huenda yakawa ni kweli kabisa kuhusu Yesu, lakini hayaelezei kiukamilifu yeye ni nani. Bibilia inatuambia yakwamba Yesu ni Mungu katika mwili, Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (tazama Yohana 1:1, 14). Mungu alikuja ulimwenguni kutufundisha, kutuponya, kuturekebisha, kutusamehe-na kufa kwa ajili yetu! Yesu Kristo ni Mungu, Muumbaji, Mungu Mkuu. Je huyu ndiye Yesu uliyemkubali?

Pili, Nini maana ya Mwokozi, na kwanini tunahitaji Mwokozi? Bibilia inatwambia yakwamba sote tumetenda dhambi; sote tufenya matendo ya uovu (Warumi 3:10-18). Kwa wajibu wa dhambi zetu, basi twastahili hasira ya Mungu pamoja na hukumu yake. Adhabu ya pekee tunayostahili kupata kwa kufanya dhambi, kinyume chake Mungu wa milele asiye na mipaka, ni adhabu isiyokuwa na mwisho au mipaka (Warumi 6:23; Ufunuo 20:11-15). Hilo tatizo ndiyo sababu tunahitaji Mkwokozi!

Yesu Kristo, alikuja duniani na akatufia pahali petu. Kifo chake Yesu, kama Mungu katika mwili, kilikuwa ni hati ya malipo isiyokuwa na mwisho kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa ili kutulipia adhabu ya dhambi zetu (Warumi 5:8). Yesu aligharimika deni letu ili wewe na mimi tusidaiwe. Kufufuka kwake Yesu katika wafu kulidhihirisha yakwamba kifo chake kilitosha kulipa adhabu ya dhambi zetu. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo pekee ndiye anayestahili kuwa Mwokozi wetu (Yohana 14:6; Matendo 4:12)! Je, wamwamini Yesu kama mwokozi wako?

Tatu, Yesu ni Mwokozi wako "binafsi"? Watu wengi huchukulia ukristo kuwa ni kuhudhuria kanisani, kufuata kanuni za ibada au kanisa, na kujitenga na dhambi fulani-fulani. Huo siyo Ukristo. Ukristo wa kweli ni ule uhusiano binafsi uliopo kati yako na Yesu Kristo. Kumkubali Yesu kama mwokozi wako binafsi inamaanisha kuweka imani yako mwenyewe kwake na kumwamini Yeye pekee. Hakuna aokokaye kupitia imani ya wengine. Hakuna asamehewaye kwa kutenda matendo fulani, hatakama ni ya wema sana. Njia ya pekee ya wokovu ni kumkubali Yesu mwenyewe kama mwokozi wa maisha yako, kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zako, na kufufuka kwake kama hakikisho lako la uzima wa milele (Yohana 3:16). Je, Yesu ni Mwokozi wako binafsi?

Kama ungetaka kumkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wako binafsi, basi yaseme maneno haya kwa Mungu. Kumbuka ya kwamba, kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee na kazi yake kamilifu pale msalabani ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Napokea ahadi yako ya msamaha na kuweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!’’

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kumkubali Yesu kama Mwokozi wako binafsi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries