settings icon
share icon
Swali

Je, Wakristo wanapaswa kujali vile wanavyoonekana kimwili?

Jibu


Mwonekano wa kimwili ni wa umuhimu kwa Mungu kwa kuwa unadhihirisha utukufu kwa uwezo wa ubunifu wake. Kwa hivyo tunapaswa kuthamini urembo ambao Mungu ametupa kama viumbe Wake wasioelezeka na waajabu. Kwa njia ambazo hatuwezi kuelewa, tunaakisi uzuri Wake mwenyewe. Mungu huweka thamani fulani juu ya mwonekano; kama hangefanya hivyo sisi sote tungefanana. Sio jambo baya kwetu kutambua na kuthamini sura ya kimwili.

Lakini lazima ikumbukwe kwamba Mungu uhukumu mioyo yetu, sio sura zetu za kimwili (1 Samweli 16:7). Ni ule mtu wa ndani ambaye ndiye kiumbe kikubwa zaidi. Tuko na nafsi ambazo kamwe hazitaaribiwa, zinaendelea kuishi milele mbinguni au kuzimuni. Mioyo yetu, pia ina uwezo wa mawazo na hisia nyingi sana, tafakari za ukuu wa Mungu usioelezeka. Tusianguke katika mtego wa kuamini kwamba mwonekano wetu unafaa kuwa chanzo cha kiburi na wivu wetu. Uzuri wetu wa kweli unapaswa utoke ndani na sio uzuri wa nje ambao ulimwengu huangalia. Katika 1 Petro 3:3-5, Petro anawaambia wake kwamba, “Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu. Kwa kuwa hivi ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu. Wao walikuwa ni watiifu kwa waume zao.”

Mwonekano wetu wa nje usiwe ndio lengo letu. Ikiwa sababu yetu ya kujaribu kuwa wakamilifu, kuvaa mavazi mazuri, kuwa na mapambo ya uso, nk, ni kuvutia watu wengine, basi sura yetu ya kimwili imekuwa ya kiburi. Tunapaswa kufahamu kwa unyenyekevu mwonekano wetu badala ya kutaka kufanana viwango vya ulimwengu. Mathayo 23:12 inasema, “Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa”. Na Yakobo 4:6 inasema, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

Lazima tuwe waangalifu kwa chochote kinachotavuta mbali na Mungu, ikiwa ni pamoja na msisitizo wa mara kwa mara ambao ulimwengu unaweka juu yetu. Mungu hataki tupende ulimwengu au kitu chochote ndani yake (1 Yohana 2:15), na hatustahili kufikiria jinsi ulimwengu unafikiria (Warumi 12:2). Mungu ametuonyesha nguvu yake ya ajabu na uzuri na upendo katika uumbaji mbali mbali. Tunapaswa kuwa wenyenyekevu, tusifanye ibada ya sanamu katika kuabudu viumbe badala ya Muumba (Wakolosai 3:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Wakristo wanapaswa kujali vile wanavyoonekana kimwili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries