settings icon
share icon
Swali

Je, kunena katika ndimi ni ushahidi wa kuwa na Roho Mtakitifu?

Jibu


Kuna matukio matatu katika kitabu cha Matendo ya Mitume ambapo kunena katika lugha kunafuatana na kupokea Roho Mtakatifu- Matendo 2:4, 10:44-46, na 19:06. Hata hivyo, hafla hizi tatu ndio sehemu pekee katika Biblia ambapo kunena kwa lugha ni ushahidi wa kupokea Roho Mtakatifu. Katika kitabu cha Matendo, maelfu ya watu wanamwamini Yesu na hakuna mahali kumesungumziwa kuhusu kunena kwa lugha (Matendo 2:41, 8:5-25, 16:31-34, 21:20). Katika Agano Jipya inafundishwa kwamba kunena kwa lugha ni ushahidi tu mtu imepokea Roho Mtakatifu. Kwa kweli, Agano Jipya hufundisha kinyume. Tunaambiwa kwamba kila muumini katika Kristo ana Roho Mtakatifu (Warumi 8:9, 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 1:13-14 ), lakini si kila muumini hunena lugha ngeni (1 Wakorintho 12:29-31).

Hivyo, kwa nini kuzungumza katika lugha kulikuwa ushahidi wa Roho Mtakatifu katika hivyo vifungu vitatu katika Matendo? Matendo 2 yanakili mitume wanabatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuwezeshwa na Yeye kwa kutangaza habari njema. Mitume kuliwezeshwa kusema kwa lugha nyingine (lugha ) ili waweze kushiriki kweli na watu katika lugha yao wenyewe. Matendo 10 imerekodi Mtume Petro kupelekwa kushiriki injili na watu wasio Wayahudi. Petro na Wakristo wengine wa mbeleni, kuwa Wayahudi, ingekuwa wakati mgumu kukubali watu mataifa (watu wasio Wayahudi) katika kanisa. Mungu aliwawezesha watu wa mataifa mengine kusema kwa lugha kuonyesha kuwa wamepokea Roho Mtakatifu Yule yule mitume walipokea (Matendo 10:47, 11:17).

Maitendo 10:44-47 inaeleza hiya: "Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, ni nani awazaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu walipokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi" Petro baadaye anarejelea tukio hili kama ushahidi kwamba Mungu alikuwa kweli anaokoa watu wa mataifa mengine (Matendo 15:7-11).

Kuzungumza katika lugha hakuna mahali kumewazilishwa kama kitu Wakristo wote wanapaswa kutarajia wakati wao wanampokea Yesu Kristo kama Mwokozi wao na hivyo kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Kwa kweli, kati ya matukio yote kubadilika katika Agano Jipya, ni rekodi mbili tu zinazungumzia mazingira ya kunena katika lugha. Lugha ilikuwa zawadi ya kimiujiza ambayo ilikuwa na kusudi maalum kwa muda maalum. Haikuwa na kamwe haitakuwa, ushahidi pekee wa kupokea Roho Mtakatifu.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kunena katika ndimi ni ushahidi wa kuwa na Roho Mtakitifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries