settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu aliniumba? Je, ni kwa nini Mungu akanitengeneza?

Jibu


Katika siku ya sita ya uumbaji, Mungu alifanya kitu ambacho hakuwa amefanya hapo awali. Wakati aliumba ulimwengu na kila kitu ndani yake, aliziumba kwa kunena tu (Mwanzo 1). Lakini kwa siku ya sita, alichukua mchanga na kuunda mtu. Kisha “akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7). Pumzi ya Mungu iliumba nafsi hai ya milele ndani ya mtu. Mungu aliumba binadamu kwa mfano Wake mwenyewe; hiyo ni, Adamu na Hawa walikuwa kama Yeye kuliko kitu chochote kingine ambacho alikuwa ameumba (Mwanzo 1:27). Binadamu wangeishi milele, kama vile tu Mungu. Aliwambia wanandoa wa kwanza wazae na wakaongezeke na wakaijaze nchi na kuitiisha (mstari wa 28). Aliwaumba kwa kusudi, na watu wote ambao walikuja baada yao waliumbwa pia kwa kusudi.

Vidokezo kuhusu sababu ya Mungu kutuumba ziko katika maeneo mbalimbali katika Biblia. Dokezo letu la kwanza ni katika Shamba la Edeni. Mwanzo 2:15 inasema kwamba Mungu alichukua mtu alikuwa ameumba na akamweka katika shamba ili alitunze. Mungu alikuwa ameumba mtunzaji wa nchi Yake. Alimpa mwanadamu utawala juu ya vitu vyote vingine na akampa kazi ya kufanya (Mwanzo 1:28). Kazi ya kwanza ya mwanadamu ilikuwa ni kuwapa majina wanyama wote (Mwanzo 2:19-20). Mungu angewapa wanyama majina Yeye mwenyewe, lakini alifurahia kufanya kazi na Adamu jinsi mzazi mwenye upendo anafurahia kuona mtoto wake anasoma ujuzi. Kwa hivyo tumeumbwa kufanya kazi, lakini sio kazi jinsi mara nyingi tunaifafanua. Kazi iliundwa kuwa njia ya kutimiza uzoefu wa Mungu kwa kufanya kazi kwa amani na Yeye ili kufanikisha malengo Yake.

Tunajua kutoka Zaburi 139:13-16 kwamba kila mmoja wetu tuliundwa na Mungu tungali ndani ya tumbo ya mama zetu. Sisi ni kazi Yake bora, tuliyeumbwa na Yeye kwa kusudi la kipekee (Waefeso 2:10). Mungu alihusika kwa karibu katika uumbaji wetu: “Neno la BWANA lilinijia, kusema; Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua; na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yeremia 1:4-5). Tangazo pekee linapaswa kutuzidia na ajabu. Bwana Mungu Mkuu, Muumbaji wa ulimwengu, anatuchagua binafsi na kisha kutuumba kamili jinsi anavyotaka tuwe. Maandiko yako wazi kwamba kila binadamu aliumbwa na Mungu kwa furaha Yake na kusudi Lake (Wakolosai 1:16).

Ikiwa tunaenda kutimiza kusudi letu, tunahitaji kushauri Biblia. Biblia inatuambia kuhusu Mungu ni nani, sisi ni nani, na jinsi tunapaswa kuishi maisha yetu. Watu wengi wanajaribu kutafuta kusudi katika furaha, burudani au umaarufu kwa sababu hawana ufahamu kwamba Mungu ana kusudi kubwa kwa maisha yao. Kwa huzuni wanamalizia bure na kuchanganyikiwa. Lakini hawahitajiki. Mungu ametupa Neno Lake (Biblia) iili tuweze kujifunza Yeye ni nani na sisi ni nani. Wakati tunashauri Biblia kwa mwelekeo, tumefungua ramani ambayo itatuongoza kwa kusudi letu.

Kitu moja tunajifunza ni kwamba Mungu anatupenda na amethibitisha upendo huo kwa kumtuma Mwanawe, Yesu, kuonyesha vile alivyo (Yohana 14:9). Ingawa Mungu anatupenda, dhambi zetu zimetutenga kutoka Kwake (Warumi 3:23; 6:23). Yesu alikuja duniani na akajitolea Mwenyewe katika nafasi yetu. Alichukua adabu ambayo dhambi zetu zinastahili (2 Wakorintho 5:21). Mungu alimfufua kutoka kwa waliokufa baada ya siku tatu, kuthibitisha kwamba Yesu ni Bwana juu ya kila kitu, ikiwemo kifo (Warumi 10: 9-10). Kisha Mungu aliamru kwamba kila mtu awekaye imani katika Yesu atasamehewa na kuwa katika uhusiano Naye (Yohana 3:16-18). Hivyo matamanio ya kwanza ya Mungu kwa kila mwanadamu ni kwamba tumjue Yeye kupitia Imani katika Mwanaye. Wakati tunajua Yeye ni nani, tunaweza tambua sisi ni nani.

Malengo ya Mungu kwa kila mtoto Wake ni kwamba tuchukue mfanano wa familia. Anataka tuwe kama Yesu (Warumi 8:29). Hivyo anatupa vipawa vya kiroho ambavyo vinatuwezesha kumtumikia Yeye kwa njia isiyo ya kawaida (1 Petro 4:10; 1 Wakorintho 12:7-11). Tanapojifunza kutembea kwa Amani na Mungu na kutumia vipawa vyetu kutumikia wengine, tunaishi kusudi letu.

Mungu alituumba kwa kusudi, lakini kusudi hilo litaonekana tofauti kutoka kwa kila mtu kwa sababu kila mtu ni wakipekee. Kuumbwa katika mfano wa Mungu inamaanisha kwamba tuliumbwa kuwa kioo cha utukufu wa Mungu—kioo cha kipekee ambacho kitaonesha vipengele mbalimbali vya asili Yake. Kioo hakina kusudi lingine ila kuonesha kitu kingine. Kioo hakina maana ikiwa kimefunikwa kwa matope; vile vile, wakati tumefunikwa katika dhambi na kugeuka kutoka kwa Mungu, tunaishi nje la kusudu tuliloumbiwa. Lakini wakati tunajibu kwa utoaji wa wokovu wa Mungu na kuruhusu Roho Wake Mtakatifu kutuosha, tunamgeukia Muumbaji wetu, na utukufu Wake unaonekana katika maisha yetu. Sio mwanga au urembo wetu dunia inahitaji kuona, lakini Wake (Yohana 8:12; 9:5).

Mika 6:8 inatuambia kile Mungu anatarajia kutoka kwetu: “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu ma Mungu wako.” Mungu alituumba tutembee na Yeye, tuongee na Yeye, tugundue sifa Zake, na kubariki ulimwengu kutoka kwa mtazamo huo. Kutenda kwa haki ni kujiweka wenyewe kwa viwango vya juu kuliko asili ya dhambi yetu ya zamani tuliyofuata (1 Wakorintho 10:31). Tunatafuta kujifunza amri za Mungu ili tuweze kuzitii. Kupenda huruma ni kuwa njia ya huruma yenyewe na neema ambayo ilituokoa (Tito 3:5). Tunatoa msamaha kwa wale wanatukosea na kuachia Mungu hukumu ya mwisho (1 Wakorintho 4:5). Tunatembea kwa unyenyekevu na Mungu wetu wakati tunakaa karibu Naye katika wakati mzuri na mbaya, kumshukuru kwa kila zawadi zuri na kumkimbilia tunapohisi kutishiwa (1 Wathesalonike 5:18; Methali 18:10). Tunapotembea kwa unyenyekevu na Mungu wetu, tunaweka hazina mbinguni vile tunaendelea kutafuta kujua na kufuata mapenzi yake. Kwa kuishi maisha yetu duniani kwa utukufu Wake, tunaweza siku moja tutasimama mbele Yake tukijua kwamba tumetimiza kusudi alilotuumbia (1 Timotheo 6:18-19; Mathayo 6:20; Luka 19:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu aliniumba? Je, ni kwa nini Mungu akanitengeneza?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries