settings icon
share icon
Swali

Je, ni Njia gani ya Wokovu ya Warumi?

Jibu


Njia ya Warumi ya Wokovu ni hali ya kushiriki Neno la Wokovu kwa kutumia aya kutoka kitabu cha Warumi katika Bibilia. Ni njia ya rahisi na Mwafaka yakuelezea kwanini tunahitaji Wokovu, kwanini Mungu alipeana Wokovu, ni jinsi gani tunaweza kupokea Wokovu, na niyapi matokeo ya Wokovu.

Aya ya kwanza katika Njia ya Warumi ya Wokovu ni Warumi 3:23, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Sote tumefanya dhambi. Sote tumefanya matendo yasiyo mpendeza Mungu. Hakuna mwenye Haki. Warumi 3:10-18 inaelezea kwa kina jinsi dhambi ilivyo maishani mwetu. Maandiko ya kifungu cha pili katika Njia ya Warumi ya Wokovu, Warumi 6:23, kinatuelezea kuhusu madhara ya dhambi – “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti;bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Adhabu tuliyopata kwa dhambi zetu ni mauti. Si mauti tu ya asili, bali ni mauti ya milele!

Aya ya tatu katika Njia ya Warumi ya Wokovu ya anzia mahali Warumi 6:23 ilipo achia, “bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 5:8 yasema, Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Kristo alikufa kwa ajili yetu. “Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu! Kifo Chake Yesu kilitulipia gharama ya dhambi zetu. Ufufuo wa Yesu unadhihirisha yakwamba Mungu alikubali kifo chake Yesu kama malipo ya dhambi zetu.

Aya ya nne katika Njia ya Warumi ya Wokovu ni Warumi 10:9, “kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” Kwasababu ya kifo chake Yesu kwa niaba yetu, kile tunacho hitajika kufanya ni kumwamini yeye, kuamini kifo chake kama malipo ya dhambi zetu-nasi tutaokoka! Warumi 10:13 yasema tena maneno haya, “Kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka.” Yesu alikufa ili atulipie gharama ya dhambi zetu na atuokoe kutoka mauti ya milele. Wokovu, msamaha wa dhambi, vyapeanwa kwa yeyote atakaye mwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake.

Hatua ya mwisho katika Njia ya Warumi ya Wokovu ni matokeo ya wokovu. Warumi 5:1 ina ujumbe huu wa ajabu, “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.” Kupitia kwa Yesu Kristo tunaweza kuwa na ushirika wa amani na Mungu. Warumi 8:1 yatufundisha, “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Kwasababu ya kifo Chake Yesu kwa niaba yetu, hatutahukumiwa adhabu juu ya dhambi zetu. Mwisho kabisa, tunayo ahadi ya thamani ya Mungu toka katika kitabu cha Warumi 8:38-39, “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.’’

Je, ungelipenda kuifata njia ya Warumi ya Wokovu? Kama ndio, hapa kunalo Ombi rahisi unaweza kuomba kwa Mungu. Kusema Ombi hili ni njia ya kujitambulisha kwa Mungu ya kuwa unamtegemea Yesu Kristo katika Wokovu wako. Maneno yenyewe hayawezi kukuokoa. Ni kwa imani tu ndani ya Yesu Kristo ipeanayo wokovu! “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyostahili ili kwa imani ndani yake niweze kusamehewa. Kwa msaada wako, ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako kwa ajili ya wokovu. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha wa dhambi-karama ya uzima wa milele! Amina!’’

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni Njia gani ya Wokovu ya Warumi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries