settings icon
share icon
Swali

Maana ya kuombea adui zako ni nini?

Jibu


Maeneo kadhaa katika Biblia yanatuamuru tuwaombee maadui zetu (Luka 6:27,35; Warumi 12:20). Mojawapo ya maandiko yanayojulikana kwetu ni kifungu katika Mahubiri ya Yesu kwenye mlima. Katika Mathayo 5:43-45, Yesu alisema, “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako,na, Umchukie adui yako, lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” Ni wazi kuwa Yesu anatarajia tuombee maadui zetu, lakini tunawezaje kufanya hivyo?

Jibu letu la kwanza kwa swali hilo labda sio sahihi. Tunapotendewa mabaya, tungependa kuomba kwamba maafa yawapate wanaotukosea! Tunaweza kuhimizwa kuomba zaburi za kuombea adui na kuwa na matumaini ya kuona Mungu akiwalipiza kisasi waovu, kama vile Yona alivyofanya nje ya Ninawi. Lakini hiyo si maana ya Yesu ya kuwaombea maadui zetu. Alikuwa na kitu bora akilini ambacho kitatuletea manufaa pamoja na maadui zetu.

Wakati mtu anaamua kutuumiza, matendo yetu ya kiasili ni kujilinda na kupigana. Walitusengenya; tutawasengenya pia. Walisema uongo dhidi yetu; tutawasemea uongo pia. Waliharibu sifa yetu; tutaharibu yao pia. Hata hivyo, Yesu anatuita kwenye kiwango cha juu zaidi. Alionyesha kiwango hicho kwa kukosa kulipiza kisasi kamwe wakati mtu alimfanyia mabaya. Na walimfanyia mabaya sana. Watu wake wenyewe walikataa ujumbe wake ( Yohana 1:11). Viongozi wa kidini walimdhihaki na kujaribu kumshitaki (Yohana 8:6). Familia yake ilimwonea haya na kujaribu kumzuia kuhubiri (Marko 3:21). Marafiki zake walimwacha wakati alipokuwa katika hali mbaya zaidi (Marko 14:50), na mji ambao ulikuwa unasema “Hosanna!”alipowasili ulipiga kelele ya “Msulubishe!” siku chache baadaye (Marko 15:13). Kwa hivyo, Yesu alikuwa na maadui, na aliposema tuombee maadui zetu, alikuwa anajua kenye anazungumzia.

Yesu alituonyesha mfano kamili wa kuombea maadui zetu alipokuwa akisulubiwa msalabani. Katikati ya mateso yake mwenyewe, alilia, “ Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” ( Luka 23:34). Alizungumza na Baba yake kuhusu watu waliokuwa wakimdhuru. Hakutaka uharibifu wao; Hakuomba kwa ajili ya kisasi. Aliomba wapate msamaha. Yesu alikuwa na huruma kwa watu waliodanganywa na kuamini kwamba walikuwa wanafanya jambo sahihi kwa kumuua Mwana wa Mungu. Hawakuwa wanajua kile kilichokuwa kinaendelea. Hawakuwa wanajua wanafanya makosa. Wakati Yesu alisema “ Hawajui watendalo,” alitoa ishara ya sababu muhimu ya kuzingatia tunapowaombea maadui zetu.

Maadui tunaowaombea hutuumiza kutokana na maumivu yao wenyewe. Fikra zao zinaweza kuathiriwa na shetani ( 2 Wakorintho 4:4). Mienendo yao huenda imetokana na majeraha ya zamani (Waamuzi 15:7). Matendo yao huenda yamechochewa na ushawishi wa wenzao (2 Wafalme 12:13-14).Hakuna chochote kati ya hizi kinachosamehea tabia zao au kupunguza madhara wanayosababisha, lakini inasaidia kueleza kwa nini wanafanya hivyo. Watu hufanya wanachofanya kwa sababu zao wenyewe. Sababu hizo zinaeza kosa kuwa za maana, lakini zinaonekana hivyo kwa wale wanaozishikilia. Basi tunawezaje kuwaombea wale waliotuumiza na hawajai kujaribu kamwe kurekebisha hali ?

1. Tunaweza kuomba kwamba Mungu atafungua “macho ya mioyo yenu yatiwe nuru” juu ya ukweli ( Waefeso 1:18). Wakati maadui wanajipanga dhidi yetu, wanakosa ufahamu. Wanarejesha hisia badala ya kujibu kutoka kwa Roho. Tunaweza kuomba kwamba Mungu atafungua mioyo yao kwa ufahamu ili wajifunze kutokana na makosa yao na wakue na hekima.

2. Tunapowaombea maadui zetu,tunaweza kuomba kwa ajili ya kutubu kwao. 2 Timotheo 2:25 inasema “akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli.” Ni Mungu anayeyeyusha mioyo ya kutosha kwa ajili ya kutubu. Tunapowaombea maadui zetu watubu, tunajua tunasali kulingana na mapenzi ya Mungu kwa sababu yeye pia anatamani watubu (2 Petro 3:9).

3. Wakati tunaposali kwa ajili ya adui zetu, tunaweza kuomba mioyo yetu ibaki kuwa nyororo na yenye manufaa ikiwa Bwana anataka kututumia kutekeleza mpango katika maisha ya adui zetu. “Jawabu la upole hugeuza hasira, Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu” (Mithali 15:1). Tunapojibu ghadhabu kwa ghadhabu, ubaya kwa ubaya, tunajiweka katika kiwango sawa na adui zetu. Lakini tunapojibu kwa ukarimu, upole, na rehema, hali mara nyingi hupoa ndani ya dakika. Hakuna kitu kinachowatia wasiwasi kama jibu laini kwa kitendo cha chuki na ukali. Hiyo ndiyo maana ya kugeuza shavu lingine (angalia Mathayo 5:39).Shetani anatamani ugomvi, hivyo anajaribu kuchochea hasira yetu na kutufundisha kujibu kwa namna ile ile. Tunapaswa kuomba kwamba Mungu aifanye mioyo yetu kuwa laini kwa wale wanaotukosea ili wema wake ufunuliwe kwao kupitia kwetu.

4. Tunapoomba kwa ajili ya adui zetu, tunaweza kuomba kwamba Mungu atende kazi katika maisha yao kwa sababu ya kosa hili ili kufanikisha mapenzi yake. Yesu alitufundisha kuomba, “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:10). Ni vizuri kuomba kwamba mapenzi ya Mungu yatimizwe katika hali yoyote ile. Tunapaswa kuomba mpaka tutake kile ambacho Yeye anataka.Ikiwa Yeye anataka kubariki adui yetu, tunataka hivyo pia. Ikiwa Yeye anataka tumtumikie adui yetu kwa njia fulani, basi hicho ndicho tunachotaka. Maombi ni kuunganisha mapenzi yetu na mapenzi ya Mungu; tunapokuwa tunasali kwa ajili ya maadui zetu, tunahitaji kupambana na hisia zetu hadi tupende kwa kweli yale Mungu anayotaka katika maisha yao.

Kuomba kwa ajili ya maadui zetu si jibu la asili kwa ukatili wao. Lakini tunakumbuka kwamba zamani sisi wenyewe tulikuwa maadui wa Mungu, na sasa sisi ni watoto wake. Sasa tunaweza kuombea wengine ambao bado wako mbali (Wakolosai 1:21). Kwa kufanya hivyo, tunahifadhi mioyo yetu kutokana na machungu (Waebrania 12:15). Kwa kuwaombea maadui zetu, tunakuwa kama Kristo, na tunajidumisha katika umoja na mapenzi ya Mungu, ambayo ndiyo jinsi kila binadamu alivyoundwa kuishi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maana ya kuombea adui zako ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries