settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kushinda kuwa na roho hakiki?

Jibu


Si vigumu kutambua roho hakiki. Matunda yake kwa kawaida ni dhahiri. Mtu ambaye ana roho ya hakiki amezoea kulalamika, ana mtazamo wenye kukata tamaa na maisha, kusikitikia matarajio ambayo hayajahafikiwa, kutambua kushindwa (kwa wengine zaidi kuliko kwake mwenyewe), na kuwa wa kuhukumu. Haifurahishi kuwa karibu na mwenye roho hakiki; wala si furaha kuimiliki.

Vile ilivyo kwa dhambi nyingi, kuwa na roho hakiki ni upotoshaji wa kitu ambacho Mungu alifanya kuwa kizuri—katika swala hili, kumtumainia Mungu na ukamilifu Wake. Mhubiri 3:11 inasema, “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.” Tunaishi katika ulimwengu ulioanguka, na mara nyingi tuna pupa ya kuingia katika utukufu wenye ukamilifu ambao kiasili tuliumbwa kwa ajili yake. Kwa namna fulani, ni vizuri kwamba tunaweza kuona kile kimekosekana katika ulimwengu huu; hata hivyo, ulimwengu hauko jinsi unastahili kuwa, wala hatuko vile tunapaswa kuwa. Kutambua kutojitosheleza kwa ulimwengu kunatusaidia kukiri hitaji letu la mwokozi. Lakini kuwa na roho hakiki inaweza kutufanya kipofu kwa nehema na uzuri ambao Mungu anaendelea kutupatia kila siku. Roho hakiki inaweza kuonekana pia kama upotoshaji wa utambuzi. Mara nyingi, wale wanaoshutumiwa kuwa na roho ya kihakiki wanatoa hoja sahihi. Wanatoa tu hoja zao kwa namna isiyopendeza.

Ni dhahiri kuwa roho hakiki ni haribifu, huangamiza wote, wa kupokea na kutoa uhakiki (Wagalatia 5:14-15). Biblia inazungumza dhidi ya aina hiyo ya hukumu ya kihakiki. Katika Mathayo 7:1-2 inasema, “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.” Yesu hasemi kwamba hatupaswi kupambanua au tupuuze asili ya ulimwengu ulioanguka. Pia hasemi kwamba hatustahili kamwe, kwa hali yeyote, kuhakiki mtu yeyote. Kwa kweli, Biblia inatuambia kwamba tunastahili kuhukumu vyema (Yohana 7:24). Hata hivyo, hatustahili kuhakiki na nia hasidi au kwa fahari, kwa unafiki, au kwa kujihesabia haki. Hatuwezi jifanya kwamba tuko waadilifu au tunaweza weka viwango vyetu kwa usawa na sahihi juu ya wengine. Binadamu kiasili wana mioyo ya udanganyifu (Yeremia 17:9) ambayo inaruhusu doa kipofu na ulinganishi usiofaa. Ni Mungu pekee anaweza hukumu na usahihi kamili (Waebrania 4:12; Yakobo 4:11-12; 1 Samweli 16:7; 1 Mambo ya Nyakati 8:9; Isaya 11:4; Ufunuo wa Yohana 16:13). Na utambuzi wetu uko sahihi tu wakati umetaarifiwa na asili mypa katika Kristo (2 Wakorintho 2:14-16; Yohana 16:13). Ni wakati tu tunapojinyenyekeza kwa Kristo na kuwa waaminifu kwetu wenyewe basi hukumu yetu itatumika kujenga badala ya kuharibu.

Basi tunawezaje kushinda roho ya kihakiki? Hali ya moyo wetu ni muhimu. Luka 6:45 inasema, “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.” Maneno ya kihakiki chanzo chake ni kutoka kwa moyo wa kihakiki. Na moyo wa kihakiki kwa kawaida hutoka kwa mavurugano wa uzuri wa Mungu—labda kwa sababu ya fahari au ukosefu tu wa habari kuhusu tabia ya Mungu na maana ya wokovu. Wakati tu tutaelewa upotovu wetu mbali na Mungu na kina cha uzuri Wake tunaweza tawaza uzuri kwa wengine (Warumi 3:23; 6:23; Wakolosai 2:13-15; Waefeso 2:1-10). Wale ambao wanakabiliana na roho ya kihakiki wanajua hawawezi kamwe kuishi kufikia viwango vyao wenyewe. Daima wanahukumu wengine na wao wenyewe na mara kwa mara wanakosa. Lakini Kristo anajaza ukosaji huu! Yeye ni mkamilifu na mwenye haki, na anapeana haki hiyo kwa wale ambao wanaamini ndani Yake (2 Wakorintho 5:21). Tunapofahamu vyema uzuri wa Mungu, tutakuwa na fadhili zaidi kwa wengine (2 Petro 2:1-3). Na tutakuwa wa shukrani zaidi. Kutoa shukrani ni kiuasimu kwa roho ya kihakiki.

Sehemu ingine muhimu ni maisha yetu ya kufikiria (Warumi 12:1-2; 2 Wakorintho 10:5). Badala ya kuzingatia kile kilochopotea, tunapaswa kufikiria kuhusu kile ni cha kweli, cha heshima, cha haki, safi, cha upendo, cha kustahili, cha bora sana na cha kusifiwa (Wafilipi 4:8). Hii si kusema kwamba tunapaswa kupuuza uongo, udhalimu, ubaya, au kutokamilika. Hata hivyo, hatupaswi kuzingatia sana kinyume. Paulo aliwaelekeza Waefeso kuhusu hili, “Kuku ahata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo … huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo … Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia …. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasemehe ninyi” (Waefeso 4:15-16, 29,31-32). Kwa uhakika, vitu vinaweza kuwa vyema kuliko vile vilivyo, lakini upendo unafunika dhambi nyingi (Mithali 10:12). Msamaha ni wa umuhimu wa kwanza. Kama mwili wa Kristo, tunazungumza kwa moyo wa upendo hili tuweze kujengana. Roho ya kihakiki unatumika tu kuharibu (Waefeso 4:1-3; Wagalatia 6:1-5).

Inaweza kuwa muhimu pia kijukumbusha kwamba hatujui fikira au nia ya wengine. Wakati mwingine, tabia inaonyesha kutia moyo, lakini si kila wakati. Kabla ya kutoa maneno ya kuhakiki (ikiwa kwa sauti au kimoyo moyo), tunapaswa kukatiza na kufikiria uwezekano mwingine. Je, huyu mtu kwa kweli ni mcheshi asiyejali, au pengine anapitia hali ngumu na anahitaji neema? Kanuni ya dsheria kuu inaweza kusaidia hapa.

Roho ya kihakiki inaharibu wale ambao wako karibu nasi na kutupokonya uwezo wetu wenyewe wa kufurahia maisha. Wakati tunakuwa wa uhakiki sana, tunakosa kwa uzuri ambao Mungu ameuweka katika ulimwengu huu. Baraka ndogo hupita bila kutambuliwa, na tunaacha kuwa wa shukrani. Kushinda roho ya kihakiki inahitaji shukrani, utayari wa kusamehe, ufahamu sahihi wa neema ya Mungu (ni bure!), uzingatiaji wa ndani wa mafikirio yetu na sharti kwa kushiriki ukweli katika upendo. Kushinda roho ya kihakiki ni swala la utakaso, na tuna usaidizi wa Roho Mtakatifu kwa hilo (2 Wathesalonike2:13). Tunapojiwasilisha kwa Mungu, kusoma Neno Lake, na kuomba kwa neema, tunapata kwamba roho ya kihakiki unakata tamaa ya udhibiti kwa Roho Mtakatifu wa Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kushinda kuwa na roho hakiki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries