settings icon
share icon
Swali

Je! Wanawake Wakristo wanapaswa kuvaa suruali refu?

Jibu


Iwe au isiwe kuwa wanawake Wakristo wanapaswa kuvaa suruali au jinzi ni suala la muda mrefu kati ya waumini. Pengine ni suala ambalo limepata kuangaziwa sana kuliko vile linastahili katika miongo miachache iliyopita. Uaminifu wa binti wa Mungu haupimwi hatimaye kwa mavazi anayovaa bali kwa kutembea kwake katika Roho (Wagalatia 5:16).

Kuna kifungu katika Agano la Kale ambacho wengine hukitumia kuzungumzia suala la wanawake kuvaa suarli au suruali-jinzi: “Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana Bwana Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi” (Kumbukumbu 22:5). Hii ilikuwa amri kwa Israeli kudumisha katika kudumisha tofauti za kijinsia katika mavazi yao; pili ilikuwa ni katazo dhidi ya kuvuka mipaka katika mavazi na tabia ya nguo za jinsia tafauti. Kwa kuwa hakukuwa na Mwisraeli wakati huo aliyevaa suruali- jinsia zote walivaa aina fulani za kanzu-lazima pia tujiulize jinsi hili linaweza tumika katika tamaduni mbalimbali. Kanuni ya jumla ni kwamba wanaume na wanawake wanapaswa kuvaa njia inayostahili katika tamaduni zao, na haimkatazi mwanamke kuvaa suruali ili muradi asijaribu kuonekana kama mwanaume.

Majadiliano ya neema yanafaa hapa pia. Wakristo hawako chini ya sheria; badala yake, tunahesabiwa haki kwa imani katika Kristo (Warumi 3:21-28). Muumini katika Kristo Yesu “amekufa” kwa vikwazo vya sheria. “Lakini sasa, kwa kufia kile kilichokuwa kimetufunga kwanza, tumewekwa huru kutokana na sheria ili tutumike katika njia mpya ya Roho, wala si katika njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa” (Warumi 7:6). Muumini haishi kwa kuifuata sheria, wala kwa hati/leseni, bali kwa neema.

Biblia haina amri inayoongoza mavazi hususani ambayo mwanamke anapaswa kuvaa. Hakuna kifungu kinachotaja nguo, sketi, suruali, kuwa inahitajika au kukataliwa. Hoja katika Maandiko ni kuvaa ipasavyo na vile vile kutofautisha jinsia. Paulo aliwaambia hivi wanawake Wakristo kuhusu mavazi yao: ”Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu” (1 Timotheo 2:9-10). Wanawake ambao wanamwabudu Mungu wanapaswa kuvaa ipasavyo, na mavazi yao yanapaswa kuonyesha unyenyekevu, sio kujionyesha; utaratibu, sio uzembe; na kiasi, si kutojizuia.

Suala la wanawake Wakristo kuvaa suruali linahitaji kushughulikiwa kwa neema. Kimaandiko, mwanamke anapaswa kuvaa mavazi yenye kiasi, yanayofaa jinsia yake na kwa ajili ya hali. Kunazo suruali zilizotengezwa kwa ajili ya wanawake haswa ambazo ni za heshima na sinafaa hali fulani? Naam, na wanawake Wakristo wako huru kuzivaa. Je, kunayo amri ya Kibiblia kwamba wanawake wavae suruali? La, na wanawake Wakristo wako huru kuvaa kanzu au sketi pekee, ikiwa hilo ndilo chaguo lake. Ni jabo la dhamiri ya mwanamke mbele za BWANA. “Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya” (Warumi 14:22).

Tunapozingatia mwanamke wa ndani, Mungu atamtunza mwanamke wa nje, na tunajua kwamba “Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu” (Warumi 14:12). Iwe ni yule anayevaa suruali wala yule anayevaa sketi pekee hapaswi kumhukumu dada yake katika Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wanawake Wakristo wanapaswa kuvaa suruali refu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries