settings icon
share icon
Swali

Katika kuifanya ndoa idumu-kuna malengo gani kuu?

Jibu


Mtume Paulo anasema kuwa mke “amefungwa” na sheria kwa mume wake wakati anapokuwa yu hai (Warumi 7:2). Kanuni hapa ni iwe ni mume au mke ambaye amakefu ili sheria ya ndoa ivunjwe. Hii ni amri ya Mungu, lakini katika ulimwengu wa sasa ndoa huishia talaka zaidi ya asili mia 51 ya wakati. Hiyo inamaanisha kuwa zaidi ya nusu ya wachumba wanaochukua kiapo “Hadi kifo kitutenganishe” wanakivunja kiapo hicho.

Wanandoa watafanya nini ili waakikishe kuwa ndoa yao imedumu? Cha kwanza na muimu ni utiifu kwa Mungu na neno lake. Hii ni kanuni ambayo lazima iwe katika matendo kabla ya ndoa. Mungu anasema, “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” (Amosi 3:3). Kwa Mkristo ambaye ameokoka, hii inamaanisha kuwa usianze uhusiano wa karibu na mtu yeyote ambaye si Mkristo. “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi?” (2 Wakorintho 6:14). Kama hii kanuni moja ilifuatwa, itaokoa machukizo na majanga katika ndoa nyingi baadaye.

Kanuni ingine ambayo itakinga urefu wa ndoa ni kuwa mume lazima amutii Mungu, na kumpenda, kumheshimu na kumkinga mke wake vile atafanya kwa mwili wake mwenyewe (Waefeso 5:25-31). Kanuni inayo ambatana na hii ni kwamba mke lazima amuheshimu Mungu na kumtii mume wake “kama kwa Mungu” (Waefeso 5:22). Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni picha ya uhusiano kati ya Kristo na Kanisa. Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya kanisa na anampenda, kumheshimu na kumkinga “mke wake” (Ufunuo 19:7-9).

Wakati Mungu alimletea Adamu Hawa katika ndoa ya kwanza, alimuumba kutoka kwa “nyama na mifupa” ( Mwanzo 2:21) na wakawa “mwili mmoja” (Mwanzo 2:23-24). Kuwa mwili mmoja yamaanisha zaidi ya uunganisho wa kimwili. Yamaanisha kukutana kwa mawazo na nafsi na kutengeneza kitu kimoja. Uhusiano huu wapita mbele ya hisia za mwili na ufuto wa mhemuko na kwa ulimwengu wa kiroho “umoja” ambao utapatikana kwa wanandoa wote wanapojitoa kwa Mungu na kwao wenyewe. Uhusiano huu haulengi “mimi na chanue” bali “sisi na chetu.” Hii ni mojawapo ya siri ya ndoa itakayo dumu. Kuifanya ndoa idumu hadi kifo ni jambo ambalo wahusika wote lazima walipe kipaumbele. Kudumisha uhusiano na Mungu na vilevile kuangalia kuwa uhusiano wako na mke/mume woko umedumishwa, na kwa hivyo utakuwa wa kumheshimu Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Katika kuifanya ndoa idumu-kuna malengo gani kuu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries