settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini kumfuata Kristo ni ngumu?

Jibu


Hakuna mzazi mwenye akili timamu ambaye amewahi kusema, “Laiti watoto wangu wangekuwa na tabia mbaya,” na hakujawahi kuwa na kitabu cha kibinafsi cha kujisaidia chenye kichwa How to live an Unhappy life (Jinsi ya kuishi maisha yasiyo ya furaha). Sisi wote tunataka baraka, furaha, na kutosheleka, na tunahusisha hali ya furaha na kiasi fulani cha urahisi. Yesu anaahidi baraka na utimilifu kwa wale wanaomfuata (Yohana 4:14), lakini watu wengi wameshangaa kwamba njia ya Kristo si rahisi kama walivyotarajia. Wakati fulani, kumfuata Kristo kunaweza kuwa kugumu sana.

Ukweli ni kwamba, baraka na dhiki hazitengani. Wanafunzi “Waliacha kila kitu” ili wamfuate Kristo, na Bwana akawaahidi baraka “mara mia moja” kama baraka ya malipo (Marko 10:28-30). Yesu alionya kwamba wote wanaomfuata lazima wajikane wenyewe na kubeba msalaba wake kila siku (Luka 9:23). Kwa hakika kutakuwa na ugumu, lakini ugumu ulio wa kusudi na kuongoza kwa furaha ya Bwana.

Wafuasi wa yesu pia wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa ulimwengu. “Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa” (2 Timotheo 3:12). Yesu hakuwaahidi wanafunzi wake kwamba kila kitu kitakuwa rahisi kwao; kinyume chake-Aliahidi kwamba watakuwa na majaribu katika ulimwengu huu (Yohana 16:33). “Lakini jipeni moyo” Aliwaambia “kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Sheria za Mungu za kimaadili zimeandikwa kwenye moyo wa kila mwanadamu-zikiwapa watu wote dhamiri ya kuwasaidia katika kupambanua mabaya na mema (Warumi 2:14-15). Wakati mtu anakuwa mfuasi wa Kristo, hana sheria ya Mungu tu moyoni mwake, bali pia, ana Roho Mtakatifu anayekaa ndani ili kumshurutisha kuishi kwa haki (Warumi 8:11). Hii haimaanishi kwa vyovyote kwamba Mkristo atakuwa na ufahamu zaidi wa dhambi yake binafsi na kuwa na hamu ya kweli ya kufanya yale yanayompendeza Kristo (Warumi 8:14-16).

Katika njia nyingi, ni baada ya mtu kuokolewa ndipo pambano dhidi ya dhambi linashika kazi katika maisha yake. Watu wote huzaliwa wakiwa na asili ambayo ina mwelekeo wa dhambi, ndiyo maana watoto hawahitaji kufundishwa jinsi ya kutenda maovu-hilo hutokea kwa kawaida. Mtu anapoongoka, asili ya dhambi haipotei-na hivyo mgogoro wa ndani huanza katika maisha ya kila muumini.

Mtume Paulo, ambaye alijiita “mtumwa wa Kristo,” anaandika juu ya mapambano na asili yake ya dhambi katika Warumi 7:14-25. Katika mstari wa 15 anasema, “Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia (7:15). Wakristo wanaohusika katika vita hivyo wana nia ya kweli ya kuepuka dhambi, lakini pia wana tamaa ya asili ya kujifurahisha na mwili. Huchanganyikiwa wakati wanajikuta “wanafanya yale wasiyotaka kufanya.” Na kwa kuifanya kuwa gumu zaidi, Wakristo hawataki kutenda dhambi tu, lakini wanachukia dhambi, lakini hata hivyo, bado wanatenda dhambi.

Paulo anaendelea kuandika, “Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu” (Warumi 7:17). Paulo anarejelea mgawanyiko unaosababishwa na kuzaliwa upya-Paulo ni “mtu mpya” kupitia Kristo (2 Wakorintho 5:17). Lakini bado anatenda dhambi kwa sababu dhambi ingali hai katika mwili wa mwanadamu-asili ya dhambi huendelea kuishi baada ya kuzaliwa upya (Warumi 7:18). Paulo anaita huu ugomvi wa ndani kuwa ni “vita,” mtu mpya anapopigana na mtu wa kale. Paulo aliona vita kuwa vya kufadhaisha sana kwa sababu alitaka kufanya vyema (Warumi 7:23). “Ole wangu mimi maskini,” Paulo analia katika dhiki yake (Warumi 7:24).

Kila Mkristo ambaye anajaribu kuishi kwa haki ameitwa katika uwanja huu wa vita katika maisha yake yote. Tuko katika vita vya kiroho. Lakini kwa neema na rehema, Mungu humpa muumini mwaminifu vazi zima la silaha kwa ajili ya vita (Waefeso 6:13).

Maisha ya Kikristo kamwe si rahisi, lakini magumu hayakanushi furaha. Tunamchukulia Yesu, ambaye “Basi na tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2). Mungu ametuweka huru kutoka utumwa wa dhambi. Ushindi ni wetu (2 Wakorintho 2:14). Kupitia kwa Roho Mtakatifu, waumini wanapata kutiwa moyo, nguvu ya kustahimili, na ukumbusho wa kufanywa wana katika familia ya Mungu. Tunajua kwamba “Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu” (Warumi 8:18).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini kumfuata Kristo ni ngumu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries