settings icon
share icon
Swali

Je, kumpenda Mungu ni mhemko, hisia, au uamuzi?

Jibu


Yesu alisema amri kuu zaidi ni ”Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe” (Luka 10:27; Marko 12:30; Mathayo 22:37). Katika Biblia yote imerudiwarudiwa, Mungu amewaamuru watu Wake kumpenda Yeye kwa mioyo yao yote na kumtumikia Yeye pekee (Kumbukumbu 6:5; 11:1; Yoshua 23:11). Lakini je, upendo unaweza kuamrishwa? Tutajiwezeshaje kumpenda mtu yeyote?

Kwa kuwa upendo umeamrishwa, basi lazima uwe chini ya uwezo wetu katika Kristo kupenda. Kwa hivyo, upendo ni uamuzi tunaofanya. Naam, upendo mara nyingi utaambatana na hisia, lakini hisia sio msingi wa upendo. Katika hali yoyote, tunaweza kuchagua kupenda, bila kujali jinsi tunavyohisi.

Neno la Kigiriki la “upendo” linalotumiwa kumrejelea Mungu ni agape, ambalo linamaanisha “fadhili, furaha, mapendeleo, au nia njema.” Huu ndio aina ya upendo ambao Mungu anao kwetu (Sefania 3:17; Yohana 3:16). Waraka wa Kwanza wa Yohana 4:19 inasema, “Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.” Kwa kuwa Mungu ni upendo na tumeumbwa kwa mfano wake, tunaweza kupenda kama Yeye (1 Yohana 4:16). Ameweka uwezo wake wa kupenda ndani ya mioyo yetu. Kisha anatufundisha jinsi ya kupenda kwa kuonyesha jinsi upendo halisi unavyoonekana (Yohana 15:13).

Kumpenda Mungu huanza na uamuzi. Ni mpangilio wa makusudi wa mapenzi yetu (Wakolosai 3:2). Hatuwezi kumpenda Mungu kwa kweli hadi pale tumemjua. Hata imani ya kuamini katika Mungu ni karama kutoka kwake Yeye (Waefeso 2:8-9). Wakati tunakubali dhawabu yake ya uzima wa milele katika Kristo, Mungu anatupa Roho Wake Mtakatifu (Luka 11:13; 1 Wakorintho 6:19). Roho wa Mungu anayedumu ndani ya mioyo ya waumini anaanza kukuza sifa za Mungu, ambapo ya kwanza ni upendo (Wagalatia 5:22). Mungu mwenyewe hutuwezesha kumpenda jinsi anavyostahili kupendwa (1 Yohana 4:7).

Tunapoendelea kukua katika ujuzi na ufahamu wa Mungu ni nani, tunaanza kupenda sifa ambazo zinamfafanua Yeye, kama vile hekima, ukweli, haki, na uadilifu (Zaburi 11:7; 90:12; Waebrania 1:9; 1 Timotheo 6:11). Na tunaanza kutambua zile sifa zilizo kinyume na hazivutii (Mithali 8:13; Zaburi 97:10). Kutumia muda wako pamoja na Mungu husababisha mioyo yetu kuwa na kiu ya utakatifu, na tunapata kuridhika zaidi ndani Yake, kwa sababu Yeye ndiye kielelezo kamili cha kila kitu tunachotamani. Kujifunza kumbwabudu “katika roho na kweli” (Yohana 4:24) huturuhusu kupata hisiz za kupendeza za upendo. Hisia haziumbi upendo, bali, wakati tunaamua kupend, hisia huja.

Kizuizi kimoja katika kumpenda Mungu ni kupenda njia za dhambi za ulimwengu huu. Hatuwezi kutumikia mabwana wawili (Mathayo 6:24), na pia hatuwezi kumpenda Mungu na ulimwengu kwa wakati mmoja. “Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake” (1 Yohana 2:15). Waumini wengi leo hii wanapaswa kutii neno lililotolewa kwa kanisa la Efeso: “Umeuacha upendo wako wa kwanza” (Ufunuo 2:4). Wito huo ni kwa ajili ya kurudisha upendo kwa Mungu pekee.

Kikwazo kingine cha kumpenda Mungu ni akili. Akili zetu daima zinajiweka kinyume na ufahamu wa Mungu na kutoa changamoto kwa imani ambayo imekwisha weka makao yake ndani ya roho zetu (2 Wakorintho 10:5). Shaka, hamaki, kutokuelewa, na mafundisho ya uongo yote yanaweza kutunyang’anya raha ya juu kabisa ya maisha, ukaribu na Mungu (Wafilipi 3:8). Vizuizi hivi vinaweza kushindwa kupitia toba na azimio la kumtafuta Mungu zaidi ya yote (Mathayo 6:33; Yeremia 29:13). Ili kumpenda Mungu kikweli, ni lazima tuache kusisitiza kwamba Mungu ajieleze kwa kututosheleza. Tunapaswa kusulubisha kiburi chetu na haki yetu kuidhinisha njia zake na kumruhusu kuwa Mungu katika maisha yetu. Tunapotambua kwa unyenyekevu kwamba Yeye pekee ndiye anayestahili kupendwa na kuabudiwa, tunaweza kujikana na kumpenda Yeye kwa jinsi alivyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kumpenda Mungu ni mhemko, hisia, au uamuzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries