settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kuwa Mkristo mwema?

Jibu


Je! haingekuwa vyema Zaidi kama maisha ya Kikristo yangekuwa na orodha ya vitu vya kufuata? Maelekezo ya aina hiyo yangetoa maagizo ambayo tunaweza kufuata ili kuhakikisha kuwa tulikuwa “Wakristo wazuri”? mambo machache katika maisha yanaweza kufanyika hivyo. Kwa kweli, hata mapishi yaliyofuatwa vizuri wakati mwingine hutokea vibaya. Wanakosa kuhesabu athari za hali ya hewa, tofauti kidogo za viungo, kutofautiana kwa joto la tanuri, au sababu nyingine kadhaa. Na “utamu” wa ladha utakuwa kwa mlaji. Kwa hivyo ni nini kinachohitajika ili kuwa Mkristo mwema?

Wengi watasema kwamba inamaanisha kwamba kusoma Biblia yako kila siku, kuomba angalau mara mbili kwa siku, kutumika kanisani, kutoa zaka, kusaidia mmishenari, kueneza Injili, na kadhalika. Hizi zote ni shughuli kuu kwa Wakristo, lakini sio kile maisha ya Kikristo yaliko.

Mkristo ni yule mtu ambaye amefanywa upya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17) na kurejeshwa katika uhusiano na Mungu. Maisha ya Kikristo yanahusu kumjua Mungu, kumfurahia, na kumletea utukufu (Isaya 43:7; 2 Wakorintho 3:18; Yohana 17:1-5,22). Ni kweli kwamba tunapomjua Mungu, kwa kawaida matendo fulani yatatokea. Yesu alisema, “Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru” (Yohana 15:14). Lakini kabla ya hayo alisema, “Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima... Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda… Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili” (Yohana 15:1-11). Utiifu-kuishi maisha ya “Mkristo mwema ”hutoka katika uhusiano wa upendo. Na utiifu utatusaidia kukaa katika upendo wa Mungu na kwa hiyo kupata furaha yake.

Kuwa “Mkristo mwema” sio kutenda matendo fulani. Bali inahusu kukua katika upendo kwa ajili ya Kristo na kumruhusu Roho wake Mtakatifu kubadilisha mioyo na maisha yetu. Yesu ndiye mwanzilishi na mkamilishi wa imani yetu (Waebrania 12:2), mwandishi wa vielekezi na ladha-mtia ladha maisha yetu. Tunapotafuta kumjua Mungu na kumtukuza, tunapata pia kumfurahia (Zaburi 73:25-26). Mkristo mwema anamjua Mungu, anamfurahia Mungu, na kukua katika neema.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kuwa Mkristo mwema?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries