settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anataka nifanye nini?

Jibu


Tunauliza swali ni nini Mungu anataka nifanye? Kwa sababu mbalimbali. Tunaweza kuwa tunakabiliwa na uamuzi mkubwa wa kufanya maishani na tunataka kufuata mpango wa Mungu. Au tunaweza kuwa tunamtafuta Mungu na kuamini kwamba kuna hatua za kufuata au sheria za kufuata ili tumpate. Au tunaweza kuuliza, “Mungu anataka nifanye nini?” kwa sababu hatuwezi pata kusudi au maana katika maisha yetu na kushuku kuwa Mungu anaificha kutoka kwetu. Chochcote kinachochochea swali hilo, Biblia ina majibu tunapojiuliza kile Mungu anataka tufanye.

Wakati unauliza mungu anataka nifanye nini, kumbuka kwamba sisi sio kazi ya binadamu. Tuliumbwa katika mfano wa Mungu kama wanadamu ili tuwasiliane na tutembee pamoja naye (Mwanzo 1:27). Kufanya ni matokeo ya kuwa. Ndege huimba kwa sababu wao ni ndege; hawaimbi ili wawe ndege. Wanaimba, wanaruka, na kunyoosha viota vyao kwa sababu ya wao ni nani. Kwa hiyo kile ambacho Mungu anataka sana ni kwamba matendo yetu yote yatoke kwenye nafsi zetu. Hapendezwi na matendo ya kinyongo ambayo hayana uhusiano wowote na mioyo yetu (Zaburi 51:16-17; 1 Samweli 15:22; Mika 6:6-8). Chochote tunachomfanyia Mungu lazima kitoke mahali pa upendo mweingi, ibada, na kujisalimisha (Hosea 6:6; 12:6).

Jambo la kwanza Mungu anataka tufanye ni kukubali toleo lake la wokovu. Hatuna tumaini katika dhambi zetu na hatuwezi kuwa wazuri vya kutosha kushinda dhambi zetu na kuingia katika uwepo Wake. Ndiyo maana Yesu alikuja ulimwenguni kuchukua ahdabu tunayostahili (2 Wakorintho 5:21). Wakati tunaiweka imani yetu katika kifo na kufufuka kwa Kristo, tunaweza kutimiza kusudi letu la kumjua Mungu (Warumi 6:1-6). Mungu anaendeleza kazi ya kutubadilisha ili tufanane zaidi na Yesu (Warumi 8:29). Kwa hivyo jibu la kwanza kwa swali Mungu anataka nifanye nini? Ni kumpokea Mwanawe, Yesu, kama Bwana na kuanza safari ya imani.

Baada ya kuokolewa, kile ambacho Mungu anataka tufanye ni “Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen” (2 Petro 3:18). Wakati Mungu anatutwaa kwa familia Yake (Warumi 8:15), tunaanza uhusiano mpya naye unaoathiri kila Nyanja ya maisha yetu. Badala ya kufanya maamuzi ya kujifurahisha wenyewe, tunafanya maamuzi ambayo yatampendeza Bwana (2 Wakorintho 10:31). Maamuzi hayo yataungwa mkono na Biblia, yatathibitishwa kupitia ushauri wa kimungu, na kutekelezwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:16, 25).

Orodha ya haraka ya mambo ambayo Mungu anataka tufanye inapatikana katika Mika 6:8, inayosema, “Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.”

Kutenda kwa haki kunahitaji tuishi tukiwa na hisia ya mema na mabaya na kushughulika kwa unyoofu na kwa usawa na wale wanaotuzunguka. Yesu alisema hatuapaswi kuhukumu kw asura tu, bali hukumu kwa haki” (Yohana 7:24). Kufanya kile Mungu anataka tufanye, ni lazima tumpe kila mtu anachostahili, tunapaswa kuishi kwa ukweli na kamwe tusimdhulumu au kumkandamiza mtu yeyote. Tunapaswa kuwatendea watu wengine vyema jinsi na namna tungependa watutendee (Mathayo 7:12).

Kupenda rehema inamaanisha tutuoe nafasi nyingine kwa mtu ambaye hastahili. Kufanya kile Mungu anatutaka tufanye, ni lazima tufuate mfano wa Yesu kwa neema; Alikuwa na hamu ya kuonyesha rehema kwa kila mtu ambaye angetubu (Yohana 8:10-11; Luka 23:42-43). Kama Yesu, lazima tusamehe wale wanaotukosea (Mathayo 18:23-35). Tunapaswa kufurahi wakati mtu anaonyeshwa rehema, tukikumbuka jinsi Mungu ametuonyesha rehema (Luka 6:35-36).

Tunatembea kwa unyenyekevu na Mungu wetu katika kutafuta baraka na kibali chake juu ya maamuzi yetu ya maisha. Mungu hawi sehemu ya maisha yet utu, Yeye ni uhai wetu (Wagalatia 2:20). Ndio tufanye kile Mungu anataka tufanye, tunakuwa katika imani yetu, kuendelea kusalimisha zaidi na zaidi sehemu za maisha yetu kwa udhibiti wake. Kila siku tunajikana wenyewe, kuchukua misalaba yetu, na kumfuata (Luka 9:23). Ni wakati ambapo tutakapotubu dhambi zetu (1 Yohana 1:9) na maisha yetu kutoka kuabudu sanamu, udunia, na maafikiano (1 Yohana 5:21) ndipo tunaweza kutembea kwa unyenyekevu na Mungu wetu.

Mungu anataka tushawishi ulimwengu wetu kwa ujumbe wake, injili. Yesu alijibu swali ni nini Mungu anataka nifanye? Pindi tu kabla hapaa kwenda mbinguni. Maneno yake tunayaita Agizo Kuu: “Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati” (Mathayo 28:19-20). Tunafanya wanafunzi kwa kuwekeza yote ambayo Mungu ametupa katika maisha ya watu ili na wao pia wawe vile vile wakuwe kile walichoumbiwa. Wakati tunazingatia juu kile tulicho katika Kristo na kusoma Maandiko, tutajua kile Mungu anataka tufanye.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anataka nifanye nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries