settings icon
share icon
Swali

Je! Tuko na sehemu mbili au tatu? Je! Tuko na mwili, nafsi na roho- ama mwili, nafsi na roho zikiwa pamoja?

Jibu


Mwanzo 1:26-27 yaonyesha kuwa hakuna kitu ambacho kinamfanya mwanadamu kuwa tofauti na viumbe vingine. Wanadamu waliumbwa ili wawe na uhusiano na Mungu, na kwa hayo Mungu alituumbia mwili na nyama. Mwili kama kawaida unaonekana na waweza guzika: mwili wa nche, mifupa, na sehemu za ndani, na kadhalika., na utaendelea kuwepo vile mtu anavyoishi. Mwili wa ndani ni zile sehemu haziwezi kuguzika: nafsi, roho, akili, nia, dhamiri, na kadhalika. Hizi huishi hata maisha ya baadaye ya mtu.

Binadamu wote wako na mwili wa nche na ndani. Ni wazi kuwa wanadamu wote wako na mwili ulio na nyama, damu, mifupa, sahemu za ndani, na ngozi. Ingawa, ni zile sehemu za mwanadamu sizizoguzika ambazo ziko na utatanishi. Je Bibilia ya sema nini kuhusu haya? Mwanzo 2:7 yasema kwamba mtu aliumbwa na nafsi hai. Hesabu 16:22 yamwehesabu Mungu kama “Mungu wa roho” ambayo wamilikiwa na watu wote. Methali 4:23 yatwambia, “Linda nafsi yako kuliko yote uyalindayo: Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” hii inamaanisha kuwa nafsi ndio chanzo cha nia na dhamira za mwanadamu. Matendo Ya Mitume 23:1 yasema, “Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mini kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi.” Hapa Paulo anairejelea dhamira, ile sehemu ya akili ambayo inatushawishi kati ya kweli na baya. Warumi 12:2 yasema, “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii: bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza, na ukamilifu.” Aya hizi na zingine nyingi, zinaashiria sehemu mbali mbali za mwili wa ndani wa mwanadamu. Zote tuko na tabia za mwili wa nche na ndani.

Kwa hivyo, maandiko yazungumzia zaidi ya nafsi na roho. Kwa kadri, pumzi, roho, nafsi, dhamira na akili zote zimeunganika na zinahusiana. nafsi na roho kwa kuelezea ndizo msingi wa mwili wa ndani usioguzika. Mara nyingi huwa na sehemu zingine. Hii ikiwa katika mawazo, je mwanadamu ni uwili (kugaganywa katika sehemu mbili, mwili/nafsi na roho) ama utatu (kugaganywa katika sehemu tatu (mwili/pumzi/ roho). Ni ngumu kuwa sawa kabisa (kamilifu). Kuna mapishano mazuri kwa mitazamo yote. Kuu la hilo ni aya ya Waibrenia 4:12: “Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya nafsi.” Aya hii yatuambia kadri mambo mawili juu ya mjadala. Nafsi na roho zaweza kugaganywa, na ugao wa nafsi na roho ni kitu ambacho ni Mungu pekee anaweza kutambua. Kuliko kuangazia kitu ambacho hatuwezi kukijua kwa hakika, ni muhimu kuangazia muumbaji, aliyetuumba “Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha” (Zaburi 139:14)

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tuko na sehemu mbili au tatu? Je! Tuko na mwili, nafsi na roho- ama mwili, nafsi na roho zikiwa pamoja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries