Swali
Ni nini maana ya uchaguzi wa tangu asili? Je! Uchaguzi wa tangu asili ni wa kibibilia?
Jibu
Warumi 8:29-30 yatuambia, “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili. Hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Waefeso 1:5 na 11 zatangaza, “Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake…. Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.” Watu wengi wako na uadui kwa kanuni ya uchaguzi wa tangu asili kuwa si kanuni ya kibibilia. La muimu ni kuelewa maana ya uchaguzi wa tangu asili kibibilia.
Neno ambalo limetafsiriwa “amuliwa” katika maandiko ambalo limerejelewa hapo juu limetoka kwa neno la Kuyunani proorizo, ambalo linabeba maana ya “kuamuliwa kabla ya” “kuchaguliwa.” Kwa hivyo, kuamuliwa ni Mungu mwenyewe kufanya uamuzi wa vitu vingine kutokea kabla ya wakati. Ni nini hiki Mungu alikiamua kabla ya wakati? Kulingana na Warumi 8:29-30, Mungu aliamua kuwa watu wengine watabadilishwa kwa mfano wa Mwanawe, waitwe waliotakasika na kuwa na utukufu. Kawaida, Mungu aliamua kuwa watu wengine wataokolewa. Maandiko mengi yawaita wanaomwani Kristo kuwa wamechaguliwa (Mathayo 24:22,31; Mariko 13:20, 27; Warumi 8:33, 9:11, 11:5-7, 28; Waefeso 1:11; Wakolosai 3:12; 1 Wathesalonike 1:4; 1 Timotheo 5:21; 2 Timotheo 2:10; Tito 1:1; 1 Petero 1:1-2; 2 Petero 1:10). Uamuzi wa asili ni kanuni ya kibibilia kwamba Mungu kwa uweza wake aliwachagua watu wengine kuokolewa.
Uadui wa pamoja kwa kanuni ya uamuzi wa asili ni kwamba si wa usawa. Ni kwa nini Mungu awachague watu wengine na awaache wengine? Kitu cha maana kukumbuka ni kwamba hakuna anayestahili kuokolewa. Wote tumetenda dhambi (Warumi 3:23), na wote tunastahili hukumu ya milele (Warumi 6:23). Kwa sababu hii, Mungu kwa ukamilifu atakua haki kwa kuturuhusu kukaa milele yote jahannamu/motoni. Ingawa, Mungu aliamua kuokoa baadhi yetu. Yeye sio Mungu aisye na haki kwa wale hawakuchaguliwa, bali wanapokea wanayostahili. Mungu kwa kuchagua kuwa mwenye huruma kwa wengine sio haki. Hakuna yeyote anayestahili kitu chochote kutoka kwa Mungu; kwa hivyo hakuna atakeye pinga ikiwa hajapokea kitu chochote kutoka kwa Mungu. Kielelezo kizuri kitakuwa mtu anawakopesha pesa watu watano katika mkusanyiko wa watu ishirini. Je! Kumi na watano ambao hawakupokea pesa watahudhika? Pengine. Je! Wako na haki ya kuhudhika? La hasha, hawana. Kwa nini? Kwa sababu huyo mtu hakuwa na deni ya yeyote. Ni vile aliamua kuwa mkarimu kwa wengine.
Kama Mungu anaamua ni nani ataokolewa, je! Hiyo haikandamizi huru wa hiari yetu kuamua kama tutamwamini Kristo? Bibilia inasema kwamba tuko na hiari- wale wote wamemwamini Kristo wataokolewa (Yohana 3:6; Warumi 10:9-10). Bibilia haijamweleza Mungu kuwa anamkataa mtu yeyote anayemwamini au mtu anayemgeuza mtu yeyote amtafutaye (Kumbukumbu La Torati 4:29). Kwa namna Fulani, kwa fumbo la Mungu, uchaguzi/uamuzi wa tangu asili wafanya kazi sako kwa bako na mtu ambaye amevutwa na Mungu (Yohana 6:44) na kuamini kwa wokovu (Warumi 1:16). Mungu aliamua ni nani atakayeokolewa, na ni lazima tumchague Kristo ili tuokolewe. Hoja zote ni kweli kwa usawa. Warumi 11:33 yasema, “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!”
English
Ni nini maana ya uchaguzi wa tangu asili? Je! Uchaguzi wa tangu asili ni wa kibibilia?