settings icon
share icon
Swali

Ni jinsi gani ukuu wa Mungu unafanya kazi pamoja na hiari huru?

Jibu


Haiwezekani kwetu kuelewa kikamilifu uhusiano kati ya ukuu wa Mungu na hiari na jukumu la mwanadamu. Ni Mungu tu pekee anajua jinsi wanavyofanya kazi pamoja katika mpango Wake wa wokovu. Kwa hili fundisho, hasa zaidi ya lingine lolote, ni muhimu kukubali kutoweza kwetu kufahamu kikamilifu asili ya Mungu na uhusiano wetu naye. Kupita mipaka kunasababisha ufahamu potovu wa wokovu.

Maandiko yako wazi kwamba Mungu huamua ni nani atakayeokolewa (Warumi 8:29; 1 Petro 1:2). Waefeso 1:4 inatuambia kwamba Mungu alituchagua “kabla ya kuumbwa ulimwengu.” Mara kwa mara Biblia inaelezea waumini kuwa “waliochaguliwa” (Warumi 8:33; 11:5; Waefeso 1:11; Wakolosai 3:12; 1 Wathesalonike 1:4; 1 Petro 1:2, 2:9) na “wateule” (Mathayo 24:22, 31; Marko 13:20, 27; Warumi 11:7; 1 Timotheo 5:21; 2 Timotheo 2:10; Tito 1:1; 1 Petro 1:1). Ni wazi ukweli kwamba waumini wamekwisha amuliwa tangu asili (Warumi 8:29-30; Waefeso 1:5, 11) na kuchaguliwa kwa wokovu (Warumi 9:11; 11:28; 2 Petro 1:10).

Biblia pia inasema kwamba ni wajibu wetu kumpokea Kristo kama Mwokozi. Ikiwa tutamwamini Yesu Kristo tutaokolewa (Yohana 3:16; Warumi 10:9-10). Mungu anajua ni nani ataokolewa na Mungu anachagua mwenye ataokolewa, na sisi ni lazima tumchague Kristo ili tuweze kuokolewa. Jinsi kweli hizi zinafanya kazi pamoja haiwezi eleweka na akili iliyo na kiwango (Warumi 11:33-36). Jukumu letu ni kuieneza injili kwa ulimwengu (Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Tunapaswa kuacha ufahamu wa mbeleni, kuchaguliwa, na kuamuliwa kwa awali iwe ni jukumu la mungu na tuwe watiifu katika kushiriki injili.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni jinsi gani ukuu wa Mungu unafanya kazi pamoja na hiari huru?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries