settings icon
share icon
Swali

Je! Ni vyema kuwa na urafiki wa karibu na wasio waumini?

Jibu


Kama Wakristo, inatulazimu kila mara kukabiliana na majaribu na mashambulizi ya ulimwengu unaotuzunguka. Kila kitu tunachokiona, soma, fanya, sikia, vaa mwilini mwetu, nk, hutuathiri kwa namna moja au nyingine. Ndio maana, ili kudumisha uhusiano wa karibu na Mungu, tunapaswa kuacha njia zetu za zamani za kufanya mambo-mambo tunayoyatizama kwenye runinga, njia zetu mbaya za zamani (uraibu wa pombe, kuvuta sigara, n.k.), utendaji tunaoshiriki, na watu tunaotumia muda wetu nao. Watu wamegawanywa katika makundi mawili, wale walio wa ulimwengu na mtawala wake, Shetani, na wale walio wa Mungu (Matendo 26:18). Makundi haya mawilil ya watu yameelezewa kwa maneno ya kinyume katika Biblia yote; k.m., walio gizani/walio katika nuru; walio na uzima wa milele/wale walio na mauti ya milele; wale walio na amani na Mungu/wale wanopigana naye; wale wanaoamini kweli/wale wanaoamini uongo; wale walio katika njia nyembamba ya wokovu/wale walio katika njia pana iendayo uharibifuni, na wengine wengi zaidi. Kwa wazi, ujumbe wa Maandiko ni kwamba waumini wako tofauti kabisa na wasioamini, na ni kutokana na mtazamo huu kwamba lazima tutambue ni aina gani ya urafiki tunaweza kuwa nao na wasioamini.

Kitabu cha Mithali kina mistari michache ya busara kwa waumini wanaofanya urafiki na wasioamini: “Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha” (Mithali 12:26). Tunapaswa kujiepusha na wapumbavu (Mithali 13:20; 14:7), kutoka kwa watu wanaoshikwa na hamaki kwa uepesi (Mithali 22:24), na kutoka kwa waasi (Mithali 24:21). Mambo haya yote yanawakilisha wale ambao hawajaokolewa. “Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini” (1 Wakorintho 6:14). Wakorintho wa Kwanza 15:33 inatuambia kwamba ushirika mbaya huharibu tabia njema. Wasioamini ni watumwa wa dhambi (Yohana 8:34), na Wakristo ni watumwa wa Mungu (1 Wakorintho 7:22). Ikiwa tunahusika kwa bidii (iwe ni kwa urafiki au usuhuba wa kimapenzi) na wasio Wakristo, sisi wenyewe tunajiweka kwa shida. Inaweza sababisha (na vile hufanya kila mara) Mkristo kujikwaa katika kutembea kwake na Mungu, kuanguka katika maisha ya dhambi, na kuwatoa wengine kutoka kwa Mungu (na kumwakilisha Mungu na Ukristo vibaya). Athari nyingine ya uhusiano wa karibu na wasioamini, ni tabia yetu ya kupuuza kweli ya Maandiko ili tusiwaudhi. Kunazo kweli ngumu katika Neno la Mungu, kweli kama hukumu na kuzimu. Tunapodunisha au kupuuza mafundisho haya au kujaribu kuyarahizisha, kimsingi tunamwita Mungu mwongo kwa ajili ya wale ambao tayari wameshikwa na Shetani. Huu sio uinjilisti.

Ingawa uhusiano huu wa karibu haushauriwi, hii haimaanishi kuwa tuwapuuze wasioamini. 2 Timotheo 2:24-26 inatuambia kwamba kama watumishi wa Bwana, tunapaswa kuwa wapole na tusiwe na ugomvi na mtu yeyote. Tunapaswa kuwafundisha kwa upole wale wanaopinga ukweli, na kuwa na subira kwa watu wagumu. Mathayo 5:16 inatuambia, “Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Tunapaswa kuwatumikia wasioamini ili waweze kumwona Mungu kupitia kwetu na kumgeukia kwa sifa. Yakobo 5:16 inasema kwamba kuna nguvu nyingi katika maombi ya mtu mwadilifu, hivyo yalete mahangaiko yako juu ya wasioamini kwa Mungu, naye atakusikiza.

Watu wengi wameokolewa kwa sababu ya huduma na maombi ya Wakristo, kwa hivyo usiwape kisogo wasioamini, lakini kuwa na uhusiano wa karibu wa aina yoyote na asiyeamini kwa uepesi na kwa urahisi unaweza geuka na kuwa kitu ambacho ni kuzuizi katika kutembea kwako na Kristo. Tumeitwa kuwahubiria injili waliopotea, na sio kuwa na ukaribu nao. Hakuna ubaya wowote katika kuwa na urafiki na mtu asiyeamini, lakini lengo la msingi la uhusiano kama huo linapaswa kuwa la kuwalete kwa Kristo kwa kushiriki Injili nao na kuonyesha nguvu ya Mungu ya kuokoa katika maisha yetu wenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni vyema kuwa na urafiki wa karibu na wasio waumini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries