settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu majonzi? Mkristo anawezaje kushinda majonzi?

Jibu


Majonzi hali ambayo imeenea, ambayo yawadhuru mamilioni ya watu, Wakristo na makafiri sawa. Wale wanaotezeka kutokana na majonzi wanaweza kuhisi huzuni, hasira, kukosa tumaini, uchovu, na aina ya dalili zingine nyingi. Wanaweza anza kuhisi kuwa wao ni watu bure na hata kuhisi kujinyonga, kutokuwa na hari ya kuongea na watu ambao wakati mmoja walifurahi nao. Majonzi kila mara huletwa na hali ya maisha, kama vile kupoteza kazi, kifo cha mwenzi, talaka au shida ya kimawazo kama vile kudhulumiwa au picha mbaya ya binafsi.

Bibilia inatuambia kuwa tujazwe na furaha na sifa (Wafilipi 4:4; Warumi 15:11), kwa hivyo hasa Mungu amenuia tuwe na maisha ya raha. Hii sio rahisi kwa mtu ambaye anatezeka kutokana na hali ya majonzi, lakini zaweza ponyeka kupitia kwa kipaji cha Mungu cha Maombi, kuisoma Bibilia na kutumia katika maisha, vikundi vya uzaidizi, ushirika wa Wakristo, kutubu, musamaha na ushauri. Lazima tufanye juhudi la kimawazo tuzizame ndani yetu, lakini tubadilishe mawazo yetu nche ndani. Hisia za majonzi zinaweza tatuliwa kila mara wakati wale walio na hisia za majonzi wanasongesha mawazo kutoka kwa wenyewe hadi kwa Kristo ana wengine.

Majonzi ya kiliniki ni hali ya mwili ambayo lazima itambuliwe na daktari. Huenda isisababishwe na hali mbaya za maisha, au dalili zinaweza inuliwa na nia ya mtu mwenyewe. Kinyume na chenye wengine katika jamii za Kikristo wanaamini, majonzi ya kiliniki kila mara hayasababishwi na dhambi. Majonzi wakati mwingine yanaweza sababishwa na utata wa kimwili ambao wahitajika kutibiwa na tabibu/ mshauri. Ingawa Mungu ako na uwezo wa kutibu ugonjwa wo wote. Hata hivyo, katika hali zingine, kumwona daktari kwa ajili ya majonzi haina tofauti na kumwona daktari kwa ajili majeraa

Kunavyo vitu vingine ambavyo wale wanaoteseka kutoka kwa majonzi wanaweza kufanya ili wainue wasiwasi wao. Lazima waakikishe kuwa wamedumu katika neno, hata wakati hawajihisi kufanya hiyvo. Hisia zinaweza kutuongoza kupotea, lakini Neno la Mungu linasimama imara na halibadiliki. Lazima tudumishe imani iwe ngumu katika Mungu na kushikilia hata kwa nguvu sana kwake hata wakati tunapitia majaribu. Bibilia inatuambia kuwa kamwe Mungu hawezi ruyahusu majaribu katika maisha ambayo hatuwezi kuyakimu/kuyatatua (1 Wakorintho 10:13). Ingawa kuwa na majonzi si dhambi, mtu bado anawajibika kwa madhara ya maumivu, kujumulisha kutafuta mataalumu wa kumsaidia. “Basi, kwa njia yekae yee, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamaye jina lake” (Waebrania 13:15).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu majonzi? Mkristo anawezaje kushinda majonzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries