settings icon
share icon
Swali

Je, watu weusi wamelaaniwa?

Jibu


Hapana, watu weusi hawajalaaniwa? Watu weusi waliumbwa kwa mfano wa Mungu kama vile wanadamu wa makabila mengine. Wazo kuwa watu weusi wamelaaniwa na Mungu na wamekusudiwa kimungu kuwa chini ya makabila mengine mara nyingi huitwa “laana ya Hamu,” kulingana na tukio lililonakiliwa katika Mwanzo sura ya 9. Madai mengine ni ya hapo nyuma, Mwanzo 4, yanayosema kwamba “alama ya Kaini” ambayo iliambatana na laana ya Kaini, ilikuwa ni kwamba ngozi ya Kaini ilibadilika kuwa nyeusi. Shida ni kuwa hakuna kati ya vifungu hivi vinasema jambo kuhusu kabila au rangi ya Ngozi. Wale wanaosema kwamba watu weusi wamelaaniwa na Mungu hawana msingi wa kibiblia wa madai hayo.

Katika Mwanzo 9, Hamu anamwona baba yake amelewa na kulalala uchi kwenye hema lake (Mwanzo 9:20-22). Hamu anawaambia ndugu zake kuhusu hali ya baba yao na ndugu hao waligeuza macho yao na kwa heshima wakamfunika baba yao (Mwanzo 9:23). Wakati Nuhu alipogunndua kilichotokea alimlaani Kanaani, mmoja wa wana wa Hamu: “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.” (Mwanzo 9:25).

Wazao wa hamu kulingana na Biblia, walijumuisha Waashuri, Wakanaani, Wamisri, na Wahabeshi (Mwanzo 10:6-20). Wanaoshikilia nadharia ya kwamba watu weusi wamelaaniwa wanaashiria ukweli kuwa wazao wa Hamu wanajumuisha Waafrika; pia wanasema kuwa jina lake Hamu, linalomaanisha “moto” katika Kiebrania, ni ushahidi kwamba watu wenye ngozi nyeusi duniani, wanaotoka katika maeneo ya joto, wote ni watoto wa Hamu na kwa hivyo ni sehemu ya laana ya Hamu. Wanatheolojia wa Kikristo wa hapo awali wakati mwingine walitumia fikra hii ili kujaribu kueleza (sio kuidhinisha) kwa nini watu wengine walikuwa watumwa mara kwa mara.

Kutamka “laana ya Hamu” ilikuwa mbinu iliyotengenezwa wakati wa kuongezeka kwa bishara ya watumwa ya Atlantiki kakika jitihada ya kuhalalisha utumwa wa rangi wa kulazimishwa. Mazungumzo ya “laana ya Hamu” yalienea sana Marekani kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo kabla na baada ya wakati huo, Wakristo wasomi walibaini kwamba mazoea ya utumwa wa rangi yalikuwa sio ya kibiblia. Ubaguzi wa rangi (Wagalatia 3:28; Ufunuo 7:9), kuteka nyara mtu (Kutoka 21:16), na utumwa wa dhuluma (Kutoka 21:20) yote yamekatazwa katika Biblia.

Hoja ya kwanza inayokanusha wazo kwamba Mwanzo 9 inafundisha kwamba watu weusi wamelaaniwa tayari imetajwa: Hakuna mahali kabila au rangi ya ngozi imetajwa katika kifungu hicho. Pili, laana ya Nuhu nidhidi ya Kanaani sio Hamu; kwa hivyo kwa maneno halisi hakuna kitu kama “laana ya Hamu” katika Biblia. Kanaani wala sio Hamu, alitabiriwa kuwa mtumwa wa ndugu yake. Wazao wengi wa Hamu hawakuwahi watumwa; kwa mfano Wamisri, wana wa Hamu, kwa muda mrefu walikuwa na hadhi ya juu kuliko ya Israeli, wana wa Shemu. Tatu, maneno ya Kiebrania yanayotumika katika Mwanzo 9:25-27 yanapatikana mukhutadha unaoashiria uduni lakini sio kazi ya kulazimishwa. Neno lilo hilo linalotafsiriwa “mtumwa” katika Mwanzo 9:25 linatumika kwa Esau na kuhusiana na Yakobo (Mwanzo27:37-40), ya Yoabu kuhusiana na Mfalme Daudi (2 Samweli 14:22), na ya Abrahamu kuhusiana na Bwana (Mwanzo 18:3). Katika visa hivi hakuna neno linalomaanisha kuwa watumwa halisi walihusika.

Utimilifu wa laana ya Nuhu kwa Kanaani ulifanyika karne nyingi baadaye wakati Waisraeli (kutoka kwa ukoo wa Shemu) waliingia katika nchi ya Kanaani na kuwatiisha wakazi wa nchi hiyo (I Wafalme 9:20-21).

Ili kukanusha nadharia kwamba mwanzo 4 inafundisha kwamba watu wa ngozi nyeusi wamelaaniwa au wanastahili kubaguliwa, tunaona maneno ya Mungu ya kukaribia Kaini: “Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi” (Genesis 4:11), na “Kisha Bwana akamwekea Kaini alama” (mstari 15). Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “alama” ni ‘owth, na hakuma mahali katika Biblia amabapo ‘owth linatumika kuashiria rangi ya ngozi. Laana juu ya Kaini ilikuwa juu ya Kaini mwenyewe; hakuna jambo limesemwa kuhusu laana ya Kaini kuendelea kwa wazao wake. Zaidi ya hayo, “alama ya Kaini” ilikusudiwa kumlinda Kaini (mstari 15) na inapaswa kuchukuliwa kuwa ni kupunguza laana, si laana yenyewe. Wazo kuwa wazao wa Kaini walikuwa na ngozi nyeusi haina msingi wa kibiblia hata kamwe. Zaidi ya hayo isipokuwa mmoja wa wake wa wana wa Nuhu alikuwa mzao wa Kaini (inawezekana lakini haionekani kuwa kweli), ukoo wa Kaini uliisha wakati wa gharika.

Kwa ufupi, madai kwamba watu wenye ngozi yeusi au watu weusi “wamelaaniwa” na Mungu yanatokana na jaribio ya kidunia ya kuhalalisha ubaguzi wa rangi. Hakuna kitu kama “laana ya Hamu” na hakuna uhalali wa utumwa wa rangi. Kinachoweka jamii dhidi ya ingine ni asili ya dhambi ya wanadamu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, watu weusi wamelaaniwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries