settings icon
share icon
Swali

Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida?

Jibu


Zaka ni dhana ya Agano la Kale. Zaka ilikuwa hitaji la sheria ambapo Waisraeli wote walipaswa kutoa asili mia kumi (10%) ya kila kitu walichomiliki-au mazao waliokuza na mifugo waliofuga-kwenye Hema la Kukutania/Hekalu (Walawi 27:30; Hesabu 18:26; Kumbukumbu 14:24; 2 Mambo ya Nyakati 31:5). Waumini katika Kristo hawajaamrishwa kutoa 10% ya mapato yao. Kila Mkristo anapaswa kuomba kwa hekima, na kutafuta hekima ya Mungu ya ni kiasi kigani anaweza kutoa (Yakobo 1:5). Watu wengi wanaamini kwambazaka ya Agano la Kale ni kanuni nzuri kwa waumini kufuata. Kutoa 10% ya mapato yako kwa Mungu kunaonyesha shukrani yako kwake kwa kila alichokupa nakukusaidia kukumbuka kumtegemea Mungu badala ya utajiri.

Biblia haisemi haswa ikiwa tunapaswa kutoa 10% ya mapato yetu yote au mapato baada ya kutozwa ushuru. Agano la Kale linafunza kanuni ya malimbuko (Kutoka 23:16; 34:22; Walawi 2:12-14; 2 Mambo ya Nyakati 31:5). Waumini wa Agano la Kale walitoa mazao bora zaidi kutoka kwa mimea yao, na sio mabakishishi. Kanuni yiyo hiyo inapaswa kutumika katika matoleo yetu hii leo. Tena, muumini anapaswa kutoa kile anachoamini kwamba Mungu anamtaka atoe. Katika yote, nia ya moyo ndio hujalisha. Je, tunatoa kwa kumcha Mungu au kwa ubinafsi kwa ajili ya mali zetu wenyewe? ”Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu” (2 Wakorintho 9:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries