settings icon
share icon

Utafiti wa Agano Jipya

Agano Jipya limegawanywa katika sehemu tano: Injili (Mathayo hadi Yohana), historia (kitabu cha Matendo ya Mitume), Nyaraka za Paulo (Warumi hadi Filemoni), Nyaraka za jumla (Waebrania hadi Yuda), na unabii (kitabu cha Ufunuo ). Agano jipya liliandikwa kutoka takribani AD 45 hadi takriban AD 95. Agano jipya liliandikwa katika kiyunani (Kigiriki, aina ya kila siku ya lugha ya Kigiriki katika karne ya kwanza AD).

Injili utupatia akaunti nne tofauti , lakini si za kutatanisha, za kuzaliwa, maisha, huduma, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo. Injili inaonyesha jinsi Yesu alikuwa Masihi aliyeahidiwa katika Agano la Kale na kuweka msingi wa mafundisho yote ya Agano Jipya. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinanakili matendo ya mitume wa Yesu, wanaume ambao Yesu aliwatuma ulimwenguni kutangaza Injili ya wokovu. Matendo ya Mitume inatwambia mwanzo wa kanisa na ukuaji wake wa haraka katika karne ya kwanza AD.Nyaraka za Paulo, zilizoandikwa na Mtume Paulo, ni barua kwa makanisa maalum - yanayotoa mafundisho rasmi ya kikristo na mazoezi yatakayofuata mafundisho hayo.Nyaraka za Jumla zinapongeza Nyaraka za Paulo na mafundisho ya ziada na matekelezo. Kitabu cha Ufunuo kinatoa unabii wa matukio ambayo yatatokea katika nyakati za mwisho.

Utafiti wa Agano Jipya ni utafiti wa nguvu na masomo ya kuzawadi. Agano Jipya linatwambia juu ya kifo cha Yesu juu ya msalaba kwa ajili yetu - na nini mwitikio wetu kwa kifo chake unapaswa kuwa. Agano Jipya inalenga kutoa mafundisho imara ya kikiristo pamoja na matokeo ya vitendo vitakavyofuata mafundisho hayo.Vifuavyo ni viungo kwa muhtasari wa vitabu mbalimbali vya Agano Jipya. Tunamatumaini kuwa utapata utafiti wetu wa Agano Jipya kuwa wa manufaa katika kutembea kwako na Kristo.

Injili ya Mathayo

Injili ya Marko

Injili ya Luka

Injili ya Yohana

Kitabu cha Matendo

Kitabu cha Warumi

Kitabu cha 1 Wakorintho

Kitabu cha 2 Wakorintho

Kitabu cha Wagalatia

Kitabu cha Waefeso

Kitabu cha Wafilipi

Kitabu cha Wakolosai

Kitabu cha 1 Wathesalonike

Kitabu cha 2 Wathesalonike

Kitabu cha 1 Timotheo

Kitabu cha 2 Timotheo

Kitabu cha Tito

Kitabu cha Filemoni

Kitabu cha Waebrania

Kitabu cha Yakobo

Kitabu cha 1 Petro

Kitabu cha 2 Petro

Kitabu cha 1 Yohana

Kitabu cha 2 Yohana

Kitabu cha 3 Yohana

Kitabu cha Yuda

Kitabu cha Ufunuo

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Utafiti wa Agano Jipya
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries